Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akongea wakati wa
mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam hivi karibuni kuhusu sekta ya
Gesi asilia nchini. Nyuma yake mwenye laptop ni Meneja wa Sekta
Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo ukanda wa Afrika wa Benki ya
Dunia Dkt Albert Zeufack, akiwa ameong
ozana na mabalozi wa nchi kadhaa
pamoja na Timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na
inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la
Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China,
Uingereza na Ujerumani.
KUPOROMOKA kwa maadili ya Mtanzania,
kumetajwa kuporomosha hadhi ya Mtanzania ndani na nje ya nchi, na sasa
wawekezaji wanaogopa kuwaajiri.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Sefue alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akifungua warsha ya
kuwajengea uwezo wadau mbalimbali katika kuinua kiwango cha uwajibikaji
na maadili katika utumishi wa Umma, mafunzo yaliyoandaliwa na
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Mbali na raia na viongozi kukosa
maadili, imeelezwa kuwa hata vyombo vya usalama vinavyoaminiwa,
vimepoteza maadili kiasi cha kusababisha raia wema kuogopa kutoa
ushirikiano kwao.
Akielezea hadhi ya sasa ya Mtannzania
kimataifa, Balozi Sefue alisema mmomonyoko huo wa maadili umesababisha
hata pasi za kusafiria za kitanzania kutiliwa mashaka na Watanzania wote
kuonekana kama watenda maovu, huku akigusia biashara ya dawa za kulevya
inavyochafua nchi.
“Zamani pasi za kusafiri za Tanzania ili
kuwa kama bendera, ilisaidia sana kufungua milango ya biashara na
uwekezaji, lakini hivi leo pasi hizo zinatiliwa mashaka na Watanzania
wote wanaonekana ni waovu,” alisema Balozi Sefue.
Michongo Alisema mmomonyoko huo pia upo
kwa baadhi ya viongozi na hata wananchi wa kawaida, na umewafanya
wawekezaji kuanza kuogopa kuajiri Watanzania kwenye baadhi ya nafasi za
ajira.
“Wapo wawekezaji wa ndani na wa nje
nimezungumza nao na wao wana wasiwasi, wanaogopa Watanzania na hata
wanashindwa kuwaajiri kwenye baadhi ya nafasi kwa kile wanachosema,
Watanzania hawana maadili na wanapenda ‘michongo’, sasa hii ni mbaya kwa
sifa ya nchi yetu,” alisema Balozi Sefue.
Alisema si jambo baya Watanzania kuwa na mali, lakini ni vyema mali walizonazo zifahamike walivyozipata kwa njia halali au lah.
“Hatusemi kuwa na mali ni vibaya hapana,
lakini tunataka utuambie mali ulizojilimbikizia kama umezipata kwa njia
halali, kwa maana wapo wasio waadilifu waliopata mali kwa njia zisizo
halali,” alisema Balozi Sefue.
Katibu wa Viongozi wa Siasa wa
Sekretarieti hiyo, Laura Maro, alisema mmomonyoko wa maadili haupo tu
kwa baadhi ya viongozi wa umma na wananchi, bali pia kwa vyombo vya
usalama ambavyo vinaaminiwa.
Alisema wakati mwingine vyombo hivyo
vinakosa maadili kwa kutaja majina ya raia wema wanaotoa taarifa za
wahalifu au wafanyabiashara haramu, jambo linalowafanya raia kuogopa
usalama wao na kutotaja tena wahalifu.
“Maadili yameporomoka sio kwa viongozi
au wananchi pekee, bali hata kwa vyombo vya usalama ambavyo vinaaminiwa,
wakati mwingine vinakosa uadilifu…sasa tunataka maadili yarudi ili
kuijenga nchi yetu,” alisema Maro.
Tufanyeje? Balozi Sefue alikiri sio wote
ni waadilifu ndani na nje ya Serikali, hivyo mapambano ya kurejesha
uadilifu lazima yafanywe kwa ushirikiano na wadau wote, ili kurejesha
maadili nchini.
Alisema suala la kurejesha maadili si
kazi nyepesi, bali ni jambo linalohitaji ushirikiano kuanzia ngazi ya
familia kwa watoto na wazazi kuelekezana jinsi ya kuboresha maadili na
pia kwa viongozi na watumishi wa umma.
Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti
hiyo, Jaji Salome Kaganda, alisema warsha hiyo itajenga ushirikiano na
wadau mbalimbali katika jamii, ili kupokea maoni na mapendekezo ya namna
ya kukabiliana na mmomonyoko wa maadili nchini. HABARILEO.
0 comments:
Post a Comment