MWANZA.
WAGANGA wawili wa jadi, pamoja na mfanyabiashara mmoja, wanashikiliwa na Polisi mkoani hapa baada ya kukutwa wakitaka kuuza mkono wa kulia unaoaminika kuwa ni wa binadamu. Watuhumiwa hao walinaswa baada ya mteg
o wa wiki nzima baada ya polisi kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
WAGANGA wawili wa jadi, pamoja na mfanyabiashara mmoja, wanashikiliwa na Polisi mkoani hapa baada ya kukutwa wakitaka kuuza mkono wa kulia unaoaminika kuwa ni wa binadamu. Watuhumiwa hao walinaswa baada ya mteg
o wa wiki nzima baada ya polisi kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Walikamatwa juzi saa 9 alasiri katika maeneo ya Ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo, akizungumzia tukio hilo, alisema:
“Tulipata taarifa kutoka kwa raia wema na tuliweka
mtego tukijifanya sisi ni wateja na kisha tulifanya makubaliano ya
kununua kiungo hicho kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji) ambao pia
waliwahakikishia wanunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata hata kichwa,
mikono, miguu na sehemu za siri za binadamu endapo wangezihitaji,”
alisema na kuongeza:
“Wauzaji hao walishapanga bei, walitaka wapewe
Sh100 milioni kwa kiganja cha mkono huo mmoja, lakini baada ya kufanya
mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei
na kuonyesha mkono huo.”
Konyo alisema, mkono huo uliwekwa kwenye begi na
kufungwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki kisha kuviringishwa kwenye
karatasi nyeupe ya nailoni, huku ukionyesha ubichi.
“Waliutoa baada ya kuwaonyesha fedha na papo hapo tukawatia mbaroni,” alisema Konyo.
Hata hivyo, Kamanda Konyo alisema taarifa
wanazozitoa ni za awali na kwamba hivi karibuni watatoa taarifa kamili
baada ya upelelezi wa polisi kukamilika pamoja na kuwakamata watuhumiwa
wengine zaidi.
Kamanda huyo pamoja na kuwapongeza wananchi
waliotoa taarifa zilizofanikisha mtego huo, alisema jeshi lake liko
katika harakati za kupambana na mauaji na uhalifu na tayari kikosi kazi
chake kiko katika Wilaya ya Magu kuhakikisha kinawatia mbaroni. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment