Na Hamisi Mussa
SHEIKH maarufu nchini, Ali Baswalehe ameondolewa katika nafasi ya
uenyekiti wa Msikiti wa Idrissa uliopo Kariakoo, Dar es Salaam kwa
tuhuma mbalimbali, ikiwemo ya kutoit
isha vikao kwa mujibu wa katiba ya
msikiti huo.
Ilidaiwa kuwa, Sheikh Baswalehe aliondolewa katika Msikiti wa Idrissa
kwa madai kuwa, amekuwa akikaa na fedha za msikiti nyumbani kwake,
jambo ambalo linatia mashaka waumini na viongozi wa msikiti huo.
Taarifa ambazo zimelifikia gazeti hili jijini Dar es Salaam zilieleza
kuwa, Sheikh Baswalehe aliondolewa katika msikiti huo ili kuunusuru.
Sheikh Baswalehe anadaiwa kuwa, ni swahiba mkubwa wa Katibu wa Shura ya
Maimamu, Sheikh Issa Ponda.
Hata hivyo, taarifa zaidi zinadai kuwa, Sheikh Baswalehe amekuwa
akitumia fedha za msikiti huo kinyume cha utaratibu na kibaya zaidi,
hakuna akaunti ya msikiti, hivyo fedha zinazotolewa kama sadaka, anakaa
nazo nyumbani kwake.
Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya waumini walidai kuwa, Sheikh
Baswalehe ameondolewa katika nafasi hiyo siku za hivi karibuni na
kwamba, walitangaziwa msikitini na uongozi wa muda uliopo ambao utakuwa
madarakani kwa kipindi cha miezi sita.
Hata hivyo, waumini hao walisema kuwa, kuondolewa kwake kumesababisha
mgawanyiko, kwani baadhi yao wamebariki na wengine kupinga wakidai
hakutendewa haki.
Pia, walisema kutokana na mgawanyiko huo, uongozi wa muda katika
msikiti huo uliomba msaada wa kuulinda kutoka kwa viongozi wa Msikiti wa
Mtambani jijini humo ambao unadaiwa kuwa, umechangia kufanyika
mapinduzi ya kumng’oa sheikh huyo.
Wakati hayo yakiendelea, waumini wengine wamekuwa wakidai kuwa,
kuondolewa kwake kwenye safu ya uongozi wa Msikiti wa Idrissa ambako
alikuwa mwenyekiti kunasababishwa na kushindwa kwake kuongoza harakati
za kumsaidia Sheikh Ponda ambaye yupo mahabusu.
Akizungumzia kuondolewa kwa Sheikh Baswalehe, Katibu wa muda,
Ramadhan Waziri, alisema hakupinduliwa wala kuondolewa bali alijiondoa
mwenyewe kutokana na Katiba inavyojieleza.
Waziri alisema kuwa, moja ya mambo ya kuzingatia ndani ya Katiba ya
Msikiti wa Idrissa ni kuitisha vikao kila baada ya miezi mitatu, lakini
Sheikh Baswalehe hakufanya hivyo.
“Tangu mwaka 2006 hadi mwaka 2013 akiwa Mwenyekiti wa Msikiti wa
Idrissa, hawajahi kuitisha kikao cha aina yoyote, jambo ambalo ni
kinyume cha katiba, hivyo tunachoweza kusema hakupinduliwa, bali
utaratibu ndiyo umemuondoa,” alisema Waziri.
Alisema Sheikh Baswalehe alikuwa na jukumu la kuwaunganisha vijana wa
kamati ya msikiti, lakini alishindwa na hivyo kuzua maswali mengi.
Kuhusu fedha za msikiti, alisema katika hilo hawezi kulizungumzia kwa
undani zaidi, lakini kimsingi ni moja ya tuhuma ambazo zinaelekezwa kwa
Sheikh Baswalehe kuwa, fedha alikuwa anakaa nazo nyumbani kwake na
hawakuwa na akaunti ya benki wala chanzo chochote cha mapato ya msikiti.
Alisema wakimhoji alikuwa akiwajibu kuwa kwani akikaa nazo yeye kuna
ubaya gani? Majibu hayo ya Sheikh Baswalehe yanadaiwa kuwa chachu ya
kuondolewa, kwani baadhi ya waumini wa msikiti walitaka kujua iwapo
atatangulia mbele ya haki fedha za msikiti nani atakuwa nazo.
Pia, alisema kikao cha kujadili uongozi wake kilifanyika Septemba 29,
mwaka huu, baada ya swala ya magharibi, ambapo Sheikh Baswalehe
alikuwepo, hivyo anafahamu.
Hata hivyo, Waziri alisema kuwa, upo ushahidi na taarifa kamili
ambayo imeandaliwa na viongozi wa msikiti huo kwa maana hiyo, hatakuwa
mzungumzaji wa kila jambo, lakini akashauri kuwa, gazeti hili kufiki
msikitini ili kujua kila kitu na hatua iliyochukuliwa.
“Tunaomba ukipata nafasi uje tuzungumze tukiwa tumekamilika, hiyo
itasaidia hata kujibu maswali mengine ambayo unahitaji kufahamu kutoka
kwetu kuhusu Sheikh Baswalehe,” alisema.
Pamoja na yaliyotokea, Waziri alisema kuwa, Sheikh Baswalehe ni mzee
wao, ni sheikh wao na kwamba, wanamheshimu, lakini kubwa zaidi ni
kupatikana kwa muda wa kutosha wa kulizungumzia suala hilo.
Hata hivyo, alisema kwa sasa Sheikh Baswalehe amekwenda Hijja, lakini
anafahamu kila hatua ambayo imechukuliwa na uongozi wa msikiti katika
kuondoka kwake.
Akizungumzia zaidi, alisema katiba ya msikiti huo imesajiliwa kwa
mujibu wa sheria, lakini pia msikiti huo muuondo wake wa kiungozi ni
kama taasisi ambayo wakati mwingine inaweza kuamua jambo kwa maslahi ya
msikiti na waumini wake. JAMBOLEO
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / SWAHIBA WA SHEIKHE PONDA ISSA PONDA ANG'OLEWA KATIKA NAFASI YA UENYEKITI MSIKITI WA IDRISSA-KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM, FEDHA HAWA CHANZO CHA KUONDOLEWA KWAKE.wahiba wa Ponda ang’olewa msikitini
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment