DAE ES SALAAM.
WAKATI Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe akisisitiza kuwa hesabu za Chadema ni miongoni mwa ambazo hazijakaguliwa, chama hicho kimeish
utumu kamati hiyo kwa kuagiza kusitishwa kwa ruzuku kwa vyama vya siasa na kusema hatua hiyo ni ubabe.
WAKATI Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe akisisitiza kuwa hesabu za Chadema ni miongoni mwa ambazo hazijakaguliwa, chama hicho kimeish
utumu kamati hiyo kwa kuagiza kusitishwa kwa ruzuku kwa vyama vya siasa na kusema hatua hiyo ni ubabe.
Wakati Chadema wakitoa kauli hiyo, jana Zitto
alisema vyama vya siasa tisa vikiwamo Chadema, CCM na CUF vinatakiwa
kufika mbele ya PAC Oktoba 25 mwaka huu, kwa ajili ya kujieleza na
kwamba chama kitakachokaidi, sheria za Bunge zinaeleza wazi, kwamba
wahusika wanaweza kufungwa jela siku saba.
Chadema kilisema kuwa PAC kabla ya kuchukua hatua,
ilipaswa kuwapa nafasi ya kuwasikiliza viongozi wa vyama husika,
kumhoji Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Msajili
wa vyama vya Siasa ambao wameshindwa kutimiza wajibu wa kukagua hesabu
hizo kwa miaka minne.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony
Komu alisema jana kuwa, uamuzi wa PAC utaviathiri vyama kwani bajeti
zake zimezingatia kuwapo kwa ruzuku.
“Kuna vyama ambavyo vinategemea ruzuku kulipa
mishahara ya wafanyakazi wake, Chadema ingawa tuna vyanzo vingine vya
mapato, tunaitegemea kukamilisha bajeti yetu kwa fedha za ruzuku ambazo
zinatusaidia kwa asilimia 45. Ni tabia mbaya kuchukua uamuzi kwa kibabe
na kuhukumu kabla ya kutusikiliza siyo haki hata kidogo,” alisema Komu.
Alitetea chama chake kwamba kimekuwa na utaratibu
wa kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa ambapo alitoa ushahidi wa barua ya
Msajili wa Vyama vya Siasa ya April 16, 2012 ikithibitisha kwamba hesabu
zao zipo sawa baada ya kuziwasilisha katika ofisi hiyo.
“Chadema tunataka ukaguzi wa hesabu usijikite
katika fedha za ruzuku pekee bali katika vyanzo vyote vya mapato ya
vyama, tatizo CAG alitueleza kwamba anakabiliwa na upungufu wa
rasilimali watu kwa hiyo PAC walipaswa kuliangalia tatizo hilo na
kutafuta ufumbuzi,” alisema Komu.
Zitto juzi alikaririwa na vyombo vya habari
akieleza kuwa Serikali ilitoa kiasi cha Sh67.7 bilioni kama ruzuku kwa
vyama tisa vya siasa tangu mwaka 2009, lakini vyama hivyo havijawahi
kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa hesabu zake kwa msajili kama sheria
inavyoagiza.
Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema),
aliamuru Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kusimamisha utoaji
wa ruzuku hadi hapo vitakapowasilisha ripoti ya ukaguzi na makatibu wake
wakuu kuhojiwa.
Miongoni mwa vyama vilivyotajwa ni APPT-Maendeleo
lakini jana Rais Mtendaji wa Chama hicho, Peter Mziray alisema chama
chake hakijawahi kupewa kiasi cha Sh217 milioni kama inavyodaiwa na PAC.
Mziray alikiri walianza kupata ruzuku 2009 ila
inasema ilikuwa kidogo kiasi cha Sh 50,000 kwa mwezi na baadae kupanda
Sh 275,000 kwa mwezi.
Alisema kiasi walichopata kuanzia mwaka 2009 ni
kiasi cha Sh12 milioni tu. “APPT-Maendeleo haina uwakilishi bungeni kwa
hiyo haiwezi kupata kiasi hicho kikubwa cha fedha,” alisema Mziray. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment