Abiria wa gari lililonasa kulia akiwa amejishika kiuno wakati dereva wa trekta akifanya jitihada za kulinasua gari lao ili waendelee na safari ya kuelekea Morogoro mjini. PICHA/MTANDA BLOG
Trekta likijaribu kulivuta fuso bila mafanikio baada ya kunasa katika tope na kuziba barabara eneo la Kilengesi baada ya mkandalasi anayejenga daraja jipya kuchepusha barabara ambayo imekuwa kero hasa kwa kunasa vyombo vya usafiri kutokana na barabara hiyo ya muda kutotengezwa vizuri katika barabara kuu Mvuha-Kisaki halmashauri ya Morogoro. PICHA/MTANDA BLOG Trekta likivuta gari ndogo baada ya kushindwa kuvuka eneo hilo ambalo magari yenye huduma ya for 4 dreva yalikuwa yanapita. PICHA/MTANDA BLOG Gari la mkuu wa wilaya Morogor likipita katika eneo ambalo ni hatari kwa usalama wa gari. PICHA/MTANDA BLOG Gari la mkuu wa wilaya ya Morogoro likipita katika tope baada ya kuweka for 4 dreva ambapo magari ambayo hayana for 4 dreva ililazimika kuvutwa na trekta ambalo lilikuwa likitoza kiasi cha sh 5,000. PICHA/MTANDA BLOG Adha hiyo haikuwa kwa wenye magari tu bali kwa chombo kinachotumia barabara kama huyu mwendesha pikipiki akisaidiwa na watoto kuivusha pikipiki katika mtaro kutokana na fusu hilo. PICHA/MTANDA BLOG Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi akivuka katika mtaro katika eneo ambalo linajengwa daraja jipya baada ya fuso kunasa katika tope. PICHA/MTANDA BLOG Katibu Tawala wilaya ya Morogoro Alferd Shayo akivuka katika bonde. PICHA/MTANDA BLOG Gari ndogo likipita mbungani baada ya fuso hilo kunasa na kuzuia magari mengine kupita. MTANDA BLOG
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / TASWIRA YA FUSO LILILONASA KATIKA TOPE NA KUZUIA MSAFARA WA MKUU WA WILAYA MOROGORO SAID AMANZI NA KULAZIMIKA MAGARI YAKE KUPITA PORINI KATIKA KIJIJI CHA KILENGESI BARABARA KUU YA MVUHA-KISAKI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment