Na Robert Hokororo.
OKTOBA 16 kila mwaka Tanzania huungana na mataifa mengine katika kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani.
Kwa mwaka huu kaulimbiu ya maadhimisho haya ya 33, ni Kudumisha mfumo endelevu wa upatikanaji wa chakula na lishe’.
Ni dhahiri kuwa afya ya mwanad
amu hutokana na lishe bora na si bora lishe kutokana na chakula anachokula.
Chakula ni moja ya mahitaji matatu muhimu ya mwanadamu ambayo kama asipopata kwa muda mrefu atakufa tu.
Vile vile kama mwanadamu huyo asipopata chakula au lishe bora hatakuwa na afya na mwili wake hautakua.
Kama ilivyo kaulimbiu ya maadhimiho ya mwaka huu ni muhimu mwanadamu
akadumisha mifumo ya kupata chakula sanjari na utaratibu bora wa chakula
na si ili mradi tu kula.
Utaratibu wa chakula unajumuisha mpangilio wa milo mitatu kwa siku kwa maana wa asubuhi, mchana na jioni.
Kama ilivyo desturi kwa watu wengi hususan katika Ukanda wa Afrika
Mashariki, chai na vitafunwa hutumiwa asubuhi, ugali na mboga hutumiwa
mchana wakati jioni wali huliwa.
Mpangilio wa milo unapaswa uende kwa wakati na si kula chakula cha
asubuhi au kifungua kinywa mchana na cha mchana kula jioni, hii si
sahihi unavuruga utaratibu.
Katika kudhirisha kuwa chakula kina umuhimu mkubwa mwanadamu anajitahidi kutumia ardhi aliyo nayo katika kujikita katika kilimo.
Hata hivyo pamoja na umuhimu wake bado idadi kubwa ya watu duniani
wanakosa chakula bora na wengine wanashindwa kupata hata mlo mmoja.
Hii ni kutokana na sababu mbalimbali zikwemo umaskini, machafuko katika baadhi ya nchi yanayosababisha watu kuhamahama.
Takwimu za Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) zinaonesha
kuwa watu takriban milioni 870 wanakabiliwa na tishio la njaa.
Wakati watu wakikabiliwa na njaa bado kuna wengine wanatupa chakula hali inayogharimu uchumi wa dunia.
Kwa mujibu wa FAO, kutokana na utupaji huo wa chakula takriban euro bilioni 570 hupotea kila mwaka.
Linasema tani bilioni 1.3 za chakula hupotea au kutupwa kila mwaka,
huku idadi hiyo ya watu wakishinda na njaa duniani.
Katika ripoti yake
iliyotolewa makao makuu ya FAO yaliyopo mjini Roma, Italia inasema
uharibifu wa mkubwa wa chakula hauathiri tu uchumi wa dunia, bali
mazingira pia. Wakati wakifanya ununuzi wa kila siku, walaji wengi
hawajui ni kiasi gani cha chakula hutupwa.
Hata hivyo mamilioni ya tani za mchele, matunda na mbogamboga huishia katika mapipa ya kutupia taka kila mwaka.
Mkurugenzi Mkuu wa FAO, José Graziano da Silva anasema kuwa ripoti
hiyo inalitaja Bara la Asia kuwa ni kinara wa utupaji chakula duniani
Pia anashtushwa na hali hiyo huku akidokeza kuwa thamani ya chakula
kinachoharibiwa ni sawa na pato la ndani la taifa la Uswisi. Katika
mataifa yanayoendelea, ripoti hiyo inabainisha kuwa chakula kinapotea
kutokana na mavuno yasiyo na ufanisi au mazingira ya uhifadhi.
Katika mataifa tajiri matunda na mbogamboga hutupwa kutokana na
sababu za muonekano ambao hauwapendezi wanunuzi, kutokana na rangi au
ununuzi wa kupita kiasi. Asia inaongoza kwa kuharibu chakula ambapo
wastani wa kilo 100 za matunda zinatupwa kila mwaka katika mataifa
yalioendelea kiviwanda kama China, Japan na Korea Kusini.
Ili kupunguza au kutokomeza uharibifu wa chakula inatakiwa kutonunua zaidi ya kile kinachohitajika.
Njia nyingine ni kutoa kutoa chakula cha ziada kulisha watu walio
katika hatari zaidi na pia kile kisichofaa kuliwa na bianadamu ni vyema
kilishiwe mifugo. JAMBOLEO
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment