BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIGOGO WA TANZANIA WALIOFICHA FEDHA KIASI CHA SH323.4 BILIONI NCHINI USWISI KUCHUNGUZWA NA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA EURODAD, MHE ZITTO KABWE KUONGOZA UCHUNGUZI HUO..

Taarifa zilizolifikia Mwananchi Jumapili na kuthibitishwa na Zitto jana jioni zilieleza kuwa Eurodad ambao ni mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali 48 kutoka nchi 19 za Ulaya, yanayojihusisha na masuala ya kufuatilia madeni ya nchi zinazoendelea, kwa muda sasa umekuwa ukipambana na watu wanaokwepa kulipa kodi. Picha na Maktaba.

DAR ES SALAAM.
WAKATI ikisubiriwa ripoti ya uchunguzi wa Tume Maalumu iliyoundwa kwa Azimio la Bunge kuchun
guza kashfa ya vigogo walioficha Sh323.4 bilioni katika benki nchini Uswisi, Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo (Eurodad), leo linaanza kuwachunguza walioficha mabilioni hayo ya fedha nchini humo.
Kazi hiyo ya uchunguzi inaanza leo hadi Novemba 5, mwaka huu, ambapo pamoja na mambo mengine watafanya ziara ya uchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za Ulaya.
Uchunguzi huo utafanywa na jopo la wataalamu waliobobea katika masuala ya kodi na maendeleo na wataongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.
Sakata la kashfa hiyo liliibuliwa bungeni kwa hoja binafsi ya Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwishoni mwa mwaka 2012.
Zitto alisema kwamba kiasi cha fedha kilichofichwa nchini Uswisi ni kikubwa zaidi ya hicho kilichotajwa.
Kufuatia hoja hiyo, Bunge chini ya Spika Anne Makinda liliipa Serikali kipindi cha mwaka mmoja ambacho kinaishia Oktoba mwaka huu, iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti hiyo bungeni.
Ripoti ya Tume hiyo iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge ilitolewa mwishoni mwa mwaka jana, ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, mpaka sasa tayari imewahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
Muda wa tume hiyo kufanya uchunguzi unakamilika mwezi huu na inatarajiwa katika mkutano ujao wa Bunge unaoanza Oktoba 29 mjini Dodoma, itawasilisha ripoti hiyo.
Taarifa zilizolifikia Mwananchi Jumapili na kuthibitishwa na Zitto jana jioni zilieleza kuwa Eurodad ambao ni mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali 48 kutoka nchi 19 za Ulaya, yanayojihusisha na masuala ya kufuatilia madeni ya nchi zinazoendelea, kwa muda sasa umekuwa ukipambana na watu wanaokwepa kulipa kodi.
“Mashirika haya yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa kesho Zitto atakutana na Waziri wa Fedha wa Uswisi na maofisa wa benki mbalimbali na asasi za kiserikali zilizopo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Geneva.
“Zitto pia atahudhuria mkutano wa Kamati ya Kodi ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa kodi za kimataifa ili kuzuia unyonywaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na kampuni kubwa za kimataifa,” inaeleza taarifa hiyo. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: