MAAFISA katika kisiwa kikubwa cha Sicily katika
bahari ya Meditarenia wanasema kuwa wamepata maiti 130 baada ya mashua
iliyokuwa imewabeba takriban wahamiaji 500 wa kiaf
rika kushika moto na
kuzama katika kisiwa cha Lampedusa.
Wahamiaji wakiokolewa kutoka baharini.
Takriban miili 103 imepatikana baharini na mingine zaidi kupatikana ndani ya boti iliyozama.
Inaarifiwa abiria walijirusha baharini wakati moto ulipozuka ndani ya boti.
Zaidi ya wahamiaji 150 wameokolewa.
Wengi wa wahamiaji hao walikuwa raia wa Eritrea na Somalia,kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Shughuli kubwa ya uokozi ingali inaendelea kuwatafuta manusura kwani inahofiwa mamia zaidi huenda wamefariki kutokana na ajali hiyo.
Meya wa mji huo anasema kuwa walionusurika wako hatika hali ya mshutuko na walimwambia kuwa moto mdogo uliwashwa baada ya meli kukwama na lengo lilikuwa kuitisha msaada.
Lakini alisema kuwa moto ulisambaa kupita kiasi na ikawa vigumu kuudhibiti.
Kisiwa cha Lampedusa kiko kati ya Tunisia na Sicily na kimekuwa kiingilio kikuu cha wahamiaji kuingia barani Ulaya. BBC.
0 comments:
Post a Comment