RAIS wa Gambia Yahya Jammeh
ameiambia dunia kwamba tishio kubwa linalotishia ustaarabu na utu wa
mwanadamu ni kuwepo kwa kampeni na uhamasishaji wa Ushoga na usagaji ameuambia Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wiki iliyopita.
"Wale wote wanaokuza ushoga ni kama wanataka kukomesha kuwepo kwa binadamu",aliuambia.
mkutano wa viongozi wa Dunia mjini New York kwa mujibu wa Gazeti la Huffington Post.
"Hili ni janga na sisi waislamu na waafrika tutapigana kumaliza tabia hii".
Aliongeza kwa kusema, "Ulawiti katika
namna yoyote ile ni uovu na ni kama kupambana na Mwenyezi Mungu. Hata
kama italazimishwa kwa nguvu fulani kuwa ni haki mwanadamu".
"Gambia ni nchi ya waumini dhambi na matendo ya zinaa yapo lakini Ushoga si wa kuvumiliwa
katika nchi ya Gambia", aliongeza Rais Yahya Jammeh.
katika nchi ya Gambia", aliongeza Rais Yahya Jammeh.
Awali aliwaambia mashoga waondoke nchini
Gambia au watakatwa vichwa.Mahusiano ya jinsia moja nchini Gambia ni
haramu.Mwaka 2009Jammeh aliwaambia maafisa wa jeshi waliopandishwa vyeo
kwamba, hatutahamasisha usagaji na ushoga katika jeshi, Ni mwiko katika
majeshi yetu.
"Ntamfukuza mwanajeshi yoyote atakaye
tuhumiwa kuwa Shoga au Msagaji katika Gambia. Sisi hatuna haja ya
Mashoga katika majeshi yetu", alisema Rais huyo.
0 comments:
Post a Comment