TAARIFA: DJ Rankim Ramadhan amefariki Dunia jioni hii katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Kufuatia msiba huo, Disco linalofanyika kila ijumaa Cassa Complex Hall Mikocheni litasimama mpaka litakapotangazwa.
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema azidi kuwashika wakati huu wa majonzi ya kumpoteza mpendwa wetu.
Hakika tasnia ya muziki imepata pengo kubwa, lakini ndio kazi ya mola kwani kila nafsi itaonja mauti.
Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi amina.
Endelea kufuatilia mtandao huu kwa habari za uhakika zaidi.
Asante kwa KUTUCHAGUA kwa wakati wote.

0 comments:
Post a Comment