SINGIDA.
WATU wawili akiwamo askari polisi wamekufa mkoani Singida katika tukio la kurushiana risasi na kundi la majangili katika Kitongoji cha Kirumbi, kilichoko katika Kijiji cha Kintanula wilayani Manyoni.
WATU wawili akiwamo askari polisi wamekufa mkoani Singida katika tukio la kurushiana risasi na kundi la majangili katika Kitongoji cha Kirumbi, kilichoko katika Kijiji cha Kintanula wilayani Manyoni.
Kundi hilo la majangili, linatuhumiwa kujihusisha
na vitendo vya biashara haramu ya nyara za Serikali. Tukio hilo
lilitokea Oktoba 31 mwaka huu katika operesheni kutokomeza ujangili
inayoendelea wilayani Manyoni.
Askari aliyeuawa katika tukio hilo ametajwa kuwa
ni mwenye namba G.9934 D/C Mgaka (26) wakati jangili ametambulika kuwa
ni Selemani Kimpinde, mkazi wa kijiji hicho.
Akithibitisha tukio hilo baada ya kutembelea
chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Mkuu
wa wilaya hiyo, Fatma Taofiq, alisema baada ya askari huyo kumkamata
jangili Seleman, walipanda gari na kuanza safari ya kwenda kuonyeshwa
zilipo silaha aina ya SMG.
Alisema lakini walitembea umbali wa mita 100,
kabla ya kufika kwenye eneo husika, askari hao waliamua kushuka kwenye
gari na kuanza kutembea kwa miguu.
Taofiq alisema baada ya kufika kwenye eneo ambalo
walitarajia kuonyeshwa silaha, alitokea jangili mwingine aliyekwenda
kumpora askari silaha aliyokuwanayo.
“Wakati wa purukushani kati ya askari na jangili
hilo lililomnyang’anya silaha, walijitokeza majangili wengine wawili na
kumpiga risasi askari huyo. Baada ya askari kuanguka chini akiugulia
maumivu, jangili huyo alianza kutimua mbio,” alisema.
Alisema jangili alikuwa hajawaona askari wengine
waliokuwa wamejificha nje na kwamba waliposikia mlio wa risasi, askari
aliyekuwa nyuma ya majangili hao alimpiga risasi jangili Kimpinde na
kufa papohapo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment