MBEYA.
WATU watano kati ya sita waliokuwa wakishtakiwa kwa makosa ya kuwashambilia wachezaji wa timu ya Tanzania Prisons na kuharibu gari lililokuwa limewabeba, juzi walihukumiwa kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya Sh 300,000 kila mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi katika Mahakama ya
Mwanzo jijini Mbeya baada ya kupatikana na kosa la kuharibu mali ya timu
hiyo ikiwamo kuvunja vioo vya gari baada ya kumalizika kwa mchezo kati
ya Mbeya City na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Sokoine jijini
hapa siku ya Jumanne.
Waliohukumiwa kwenda jela lakini walijiokoa kwa
kulipa faini ni Brayson Shaibu, Vicent Ramadhan, Maiko George, Emmanuel
Ndalo na Enock Jeremia wakati aliyeshinda kesi hiyo ni David Laurence.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu wa mahakama hiyo, Sadik
Mbillu alisema kuwa mahakama hiyo iliridhishwa na ushahidi uliotolewa
na upande wa mashtaka na kuwakuta na hatia watu watano kwa kosa la
kuharibu mali ya Magereza. MWANANCH.
0 comments:
Post a Comment