BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINE ZA EFDs ZAIFANYA SERIKALI KUPATA HASARA YA SH1 MIL KUTOKONA NA MGOMO WA SIKU MBILI WA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM..

Mashine za kutolea risiti za elektroniki (EfDs)

SERIKALI imepata hasara ya zaidi ya sh bilioni moja kutokana na mgomo wa wafanyabiashara wa maduka Kariakoo uliodumu kwa siku mbili.



Wafanyabiashara hao waliingia katika mgomo na kufunga maduka yao wakiilalamikia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inayosimamia utekelezaji wa matumizi ya mashine za kielektroniki ambazo wanadai gharama yake ni kubwa ukilinganisha na mapato yao.


Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa wanajumuiya hiyo aliyeomba asitajwe jina kwa kuwa si msemaji, alisema asilimia kubwa ya wateja wa benki katika eneo hilo wanategemea wafanyabiashara hao, hivyo kitendo cha kufungwa kwa maduka hayo kilichangia hasara kwa serikali na benki.


“Pamoja na serikali kupata hasara, bado wageni wa nchi mbalimbali wanaofika kupata mahitaji Kariakoo walipata hasara kubwa na hata wengine waliomba serikali ifanye haraka kutatua jambo hilo ili kuwawezesha kupata mahitaji,” alisema.


Alisema ni muhimu serikali ikatekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwa pamoja na wafanyabiashara hao kwa ajili ya kuhakikisha mgogoro huo hautokei tena.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alilazimika kusikiliza kilio chao na kuwataka waendelee na utaratibu wa zamani hadi Desemba 31 wakisubiri ufumbuzi wa serikali.


Kanuni ya mwaka 2012 ndiyo inayotumika kwa wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki (EFDs), ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, kutotumia bila sababu yeyote faini yake inakuwa sio chini ya sh milioni tatu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: