STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’, Alhamisi iliyopita alijikuta akiutibua msafara wa Rais wa
Zanzibar, Dk. Mohamed Shein kufuatia kuondoka kwenye msiba wakati
ilitangazwa kiongozi huyo ndiye aliyetakiwa kuanza kuondoka.
Ishu hiyo iliyotafsiriwa kama jeuri ya
staa huyo ilitokea Mbuzini Mjini Magharibi, Zanzibar baada ya kumalizika
kwa mazishi ya baba wa Wema Sepetu, aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania
Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Waziri wa Elimu wa zamani
katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Isaac Abraham
Sepetu.
DIAMOND AINGIA
Awali, wakati waombolezaji wamekaa
wakiusubiri mwili wa marehemu ufike, ghafla Diamond aliibuka
akisindikizwa na kundi la wapambe mpaka alipokaa.
AWEKWA MSTARI WA MBELE
Diamond alipofika aliwekwa mstari wa mbele ambako walikaa ndugu wa karibu na watoto wote wa marehemu.
MC ATANGAZA ITIFAKI YA SERIKALI
Mwili ulipowasili, ratiba ya mazishi
ikatangazwa na MC ambapo alitaja utaratibu wa mazishi mpaka watu
watakaotakiwa kuweka mashada ya maua kaburini, akiwemo Rais Shein.
Baada ya mazishi, Mwongoza Shughuli
ambaye jina halikujulikana aliwaomba watu wote wazingatie itifaki ya
usalama wa taifa kwamba ni lazima viongozi wote wa serikali waondoke
ndipo waombolezaji wengine watawanyike.
“Jamani naomba sana itifaki izingatiwe,
asiondoke mtu yeyote kabla ya viongozi wetu wa serikali, akiwemo Rais
Shein hawajaondoka,” alisema MC huyo.
DIAMOND APUUZA, ANYANYUKA
Baada ya MC huyo kutoa mwongozo, watu
wote walitulia wakisubiri kiongozi wa kwanza kuondoka ambaye alikuwa ni
Rais Shein kama itifaki ilivyotaka.
Lakini kabla Rais Shein hajaanza
kusimama, Diamond alinyanyuka na kuzua kasheshe kwa sababu baadhi ya
watu, hasa wa umri wake walianza kumkimbilia huku wakikanyagana na
kusababisha hali ya taharuki.
MC AWATULIZA WATU
Baada ya watu kuanza kukimbizana hovyo
muongozaji wa msiba huo aliwaomba watulie na kusema kuwa wasiogope ila
kuna staa ambaye anapita ndiyo maana watu wamemkimbilia.
“Naomba utulivu huyo ni staa f’lani
kapita huko ndiyo maana watu wanamkimbilia hivyo tulieni kwanza viongozi
wetu waondoke,” alisema.
USALAMA WA TAIFA NUSURA WAMKAMATE
Baada ya kuona watu wakikimbia hovyo
baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa walitaka kumkamata msanii huyo
wakisema alisimama kwa makusudi licha ya kusikia tangazo la kiitifaki.
WATU WAMSHANGAA DIAMOMD
Baadhi ya watu waliohudhuria msiba huo
walionekana kushangazwa na kitendo cha Diamond na kusema kuwa ni vyema
angesubiri viongozi wote waondoke ndipo na yeye atimke lakini kufanya
vile si sahihi.
“Huyu Diamond kwani ana nini? Nakumbuka
kwenye msiba wa Kanumba kule Dar pia aliingia kipindi ambacho
ilitangazwa kuna kiongozi anakwenda, utaratibu ukatibuka, watu wakawa
wanamshangilia yeye,” alisema mtu mmoja aliyetoka Dar kwenda Zanzibar
kumzika mzee Sepetu.
0 comments:
Post a Comment