JAPO wengine wanaweza kuwa na maana tofauti, ndoa inafahamika
kuwa ni muungano baina ya watu wa jinsi tofauti yaani mwanaume na
mwanamke.
Kwa Wakristo ndoa inapaswa kuwa ya mke mmoja na mume mmoja, wakati kwa Waislamu, mume anaruhusiwa kuoa zaidi ya mke mmoja.
Kwa Wakristo ndoa inapaswa kuwa ya mke mmoja na mume mmoja, wakati kwa Waislamu, mume anaruhusiwa kuoa zaidi ya mke mmoja.
Siku ya kuoana na hata kabla, kuna ahadi ambazo
watu hao hupeana;hasa zinahusiana na kuheshimiana na kufanya mambo yenye
lengo la kuonyesha upendo wa dhati na kuimarisha ndoa yao na familia
kwa ujumla.
Hata hivyo hapa nchini kama ilivyo katika nchi
mbalimbali za nje, kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya wanandoa
kutoheshimu viapo walivyopeana siku wanafunga ndoa.
Baadhi ya wasomi maarufu katika masuala ya ndoa,
Kertzer, David I na Marzio Barbagli (2001) wanasema katika utafiti wao
walioupa jina la the history of the European family yaani historia ya
familia Ulaya, uliochapishwa na Chuo Kikuu Yale, Marekani kuwa ndoa
njema ni ile ambayo watu wake wanajali kwa vitendo ahadi walizopeana za
kuishi vizuri. Kwa bahati mbaya kuna watu wanaingia kwenye ndoa wakiwa
wanaelewa vizuri, baada ya kuanza kuwa umaarufu au kuwa na fedha, ndoa
zao hugeuka na kuanza kuwa mbaya.
Badala ya fedha kuwa sehemu ya kusaidia maisha yaweze kuwa bora,zinaonekana kuchangia kuwa na ndoa zilizokithiri migogoro.
Wengi huanza kurudi usiku wa manani au hata kulala nje kwa visingizio vya wingi wa kazi au hata safari feki za kazi.
Watafiti Evans, Tanya (2005) katika chapisho
walilolipa jina la Women, Marriage and the Family yaani wanawake ndoa na
familia wanasema kutoheshimu ndoa kunasababisha baadhi ya watu
kushindwa kuwa na maisha bora kwa sababu ya kutumia fedha nyingi bila
sababu za maana.
“Wengine nje ya ndoa wana zaidi ya wanaume au
wanawake mmoja, hii yote ni kuonyesha namna gani si bora, kwani walio
bora hujua namna ya kuvifanya hata visivyo vizuri view vizuri” inasema
sehemu ya utafiti wa wasomi hao ikizingumzia tabia za baadhi ya watu wa
kada mbalimbali.
Hivi karibuni, Rais Robert Mugabe aliwaonya
mawaziri wake dhidi ya `nyumba ndogo’ akisema baadhi ya mawaziri
wanatumia mali zao nyingi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi wa wanawake
wasio wake zao.
Kuna viongozi wameoa wake wengine na kuachana na
wale wa awali bila sababu za maana, huku watoto wao wakiwa na maisha
duni. Kinachoonekana ni kama wake wengi wa viongozi na watu wenye fedha,
wanaishi kwenye ndoa kwa kuvumilia, siyo kwa furaha; wengi kwa nje
wanaonekana wana furaha, ndani ni shida.
Wengine hawajawahi kupanda gari pamoja na waume
zao kwenda kwenye matembezi, na hata wanapotaka ukaribu huambiwa kwani
shida ni nini kama kula si unakula…
watu hawaingii kwenye ndoa kufuata kula, bali uhusiano mzuri wenye amani, wanasema watafiti Berstein na Nina (2007) katika utafiti wao walioupa jina la “Polygamy, Practiced in Secrecy” yaani katika maana isiyo rasmi ndoa za wake wengi zinavyoendesha kwa kificho. MWANANCHI.
watu hawaingii kwenye ndoa kufuata kula, bali uhusiano mzuri wenye amani, wanasema watafiti Berstein na Nina (2007) katika utafiti wao walioupa jina la “Polygamy, Practiced in Secrecy” yaani katika maana isiyo rasmi ndoa za wake wengi zinavyoendesha kwa kificho. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment