BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UVCCM: WAMTUHUMU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF), MAALIF SEIF HAMAD KUWA NI DIKTETA.

 
Maalim Seif Sharif Hamad.

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar,  umemtuhumu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) kuwa  ni kiongozi mwenye viashiria vya udikteta.



Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, alitoa kauli hiyo juzi katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Shaka alisema kitendo cha kiongozi huyo kukataa  kuachia  madaraka ya kisiasa na kulipisha kundi la vijana ni udikteta usio na mipaka ndani na nje ya Bara la Afrika.


Alibainisha kuwa inasikitisha kusikia kiongozi huyo akitangaza kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani ilhali alishindwa mara nne katika chaguzi zilizofanyika miaka iliyopita.


“Tangu mwaka 1992 hadi leo Maalim Seif ameshikilia vyeo ndani ya CUF, amekuwa Makamu Mweyekiti wa CUF, mgombea urais  wa kudumu, sasa Katibu Mkuu na hataki kuachia ngazi ili kuwapa nafasi vijana, ndiyo maana nasema ni dikteta hatari,” alisema.


Shaka aliongeza kuwa laiti Maalim Seif angelikuwa anaheshimu misingi ya demokrasia na kutambua umri wake asingeendelea kushiriki siasa kama alivyoahidi hivi karibuni kuwa hataacha siasa hadi aishiwe nguvu.


Shaka aliwataka vijana wa CUF  kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCM ili waweze kupata nafasi ya kuonyesha uwezo  wa kushikilia nafasi za uongozi ambao sasa unahodhiwa na Maalim Seif. TANZANIA DAIMA
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: