BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VITA YA IBRAHIMOVIC NA ROBALDO KUHAMIA SWEDEN DHIDI YA NCHI ZAO KATIKA KUWANIA NAFASI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA LEO.



FILE - Portugal's Cristiano Ronaldo (L) shakes hands with Sweden's Zlatan Ibrahimovic (R) following their World Cup South Africa 2010 Group 1 qualifying soccer match between Sweden and Portugal at the Rasunda soccer stadium in Stockholm, Sweden, 11 October 2008. EPA/JONAS EKSTROMER SWEDEN OUT +(zu dpa «Auslosung Fußball-WM-Qualifikation» vom 21.10.2013) +++(c) dpa - Bildfunk+++Nyota wawili Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic.

MSOMAJI, naandika nikiwa Sweden. Leo mechi za mwisho za kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia zinachezwa. Na kesho tutajua majina ya timu zote 32 ambazo zitashiriki fainali hizo.
Katika mashindano hayo mwaka kesho, kati ya timu hizi 32 , moja itakuwa Ureno au Sweden. Leo Sweden wanacheza dhidi ya Ureno katika uwanja wao wa nyumbani hapa Stockholm.
  

Jina la uwanja ni Friends Arena. Mimi nimepata tiketi ya mechi na hivyo fursa ya kwenda uwanjani kuiona mechi ya usiku wa leo. Ijumaa iliyopita Sweden walicheza dhidi ya Ureno katika uwanja wa Estadio Da Luz nchini Ureno. Sweden walifungwa kwa goli moja kwa bila, na Ronaldo alifunga goli hilo. 


Vyombo vingi vya habari duniani vinaongea zaidi kuhusu mechi ya Ibrahimovic dhidi ya Ronaldo inapohusu mechi ya Sweden dhidi ya Ureno. Ni kwa kuwa Ronaldo na Ibrahimovic wamekuwa wachezaji bora barani Ulaya msimu huu. Na wachezaji hawa ni wachezaji muhimu zaidi katika timu zao za taifa. Ibrahimovic na Ronaldo hawachezi katika nafasi moja, lakini , wachezaji hawa wanafanana sana. 


Wachezaji hawa wote wanataka kuwa wafungaji bora katika historia ya timu zao za taifa . Ibrahimovic amefunga magoli 46 katika timu ya taifa ya Sweden , na amebakia na magoli matatu tu kumfikia Sven Rydell ambaye amefunga magoli mengi zaidi katika historia ya timu ya taifa ya Sweden.


Ronaldo amefunga magoli 44 katika timu ya taifa ya Ureno na vile vile amebakia na magoli matatu tu kufikia rekodi ya Pauleta ambaye amefunga magoli mengi zaidi katika timu ya taifa ya Ureno.


Zamani Ronaldo na Ibrahimovic walisemwa kwa sababu hawakupiga pasi nyingi za magoli wakiwa uwanjani , na kwamba walitaka zaidi wafunge wenyewe tu , na pia walipenda kupiga chenga tu badala ya kuzisadia timu zao. 


Leo Ronaldo na Ibrahimovic watatumia uwezo wao wote kuhakikisha kwamba timu zao zinashinda badala ya kuhakikisha kwamba wao wanafunga magoli. Kwa sasa Ronaldo na Ibrahimovic hawafungi tu magoli mengi lakini , wanapiga pasi nyingi za magoli pia. Na ndio mana wachezaji hawa ni manahodha katika timu zao za taifa.


Usiku huu mmoja kati ya Ronaldo na Ibrahimovic ataipeleka timu yake ya taifa katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil. 


Hata kama Sweden walifungwa na Ureno katika mji wa Lissbon wiki iliyopita, Waswidi bado wanaamini kwamba timu yao
ina nafasi kubwa ya kufuzu kwenda Kombe la Dunia.



Wanaamini kwamba Zlatan Ibrahimovic atawapeleka Brazil. Tutaona... Olle Bergdahl Mjengwa Stockholm. Sweden.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: