Mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala
Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.
Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu
nyingine.(P.T).
Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu
nyingine.(P.T).
Dereva huyo
aliendelea kusimulia kuwa alimpeleka jamaa mpaka eneo la tukio hilo
kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.
Mara baada ya
kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha
kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati
akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba.
Wakati jamaa anaelekea getini
mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu
wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye alikuwa akiendesha gari , mama mmoja
na wadada wawili.
Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu
waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja
aliyefahamika kwa jina moja la Carol.Baada ya dreva tax kuona hali
imechafuka ilimbidi akimbie.
Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio
hilo jamaa pia alimpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na
pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.
Mtuhumiwa na dereva
aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja
akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.
Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauaji hayo licha ya watu wengi kudai kuwa ni wivu mapenzi.
0 comments:
Post a Comment