Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood kulia akimkabidhi vifaa Mwenyekiti, Theodola Thiodol (32) sehemu ya vifaa mbalimbali ikiwemo mipira na saruji yenye thamani ya sh320,000 kwa ajili ya matumizi ya kutumika katika mradi wa kupata majisafi na majisalama katika kijiji hicho kinachokabiliwa na kero ya maji kwa muda mrefu mkoani Morogoro. PICHA/MTANDA BLOG.
Mbunge
wa jimbo la Morogoro Abdullaziz Abood kulia akikabidhi vifaa mbalimbali
ikiwemo mipira na saruji yenye thamani ya sh320,000 kwa ajili ya
matumizi ya kutumika katika mradi wa kupata majisafi na majisalama
katika kijiji hicho kinachokabiliwa na kero ya maji kwa muda mrefu
mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
Wananchi wa kijiji cha Mjipya mtaa wa Vituli kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro wakiongoza na mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood (mwenye fulana nyeusi) kupandisha mlima huku baadhi ya wananchi hao wakiwa wamebeba vifaa ikiwemo mifuko ya saruji na mipira.
Na Mtanda Blog, Morogoro.
WANANCHI wa mtaa wa Mwanzomgumu kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro wamewachongea viongozi wa serikali ya mtaa huo kwa mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood huku viongozi hao wakishindwa kuitikia wito wa mbunge huyu aliyetaka kufika eneo la tukio ili kusikiliza kero zao pamoja na kuzipatia ufumbuzi mkoani hapa.
Mbunge huyo alikuwa katika ziara ya kata tatu za Manispaa hiyo za kukabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo vyerehani, mipira ya kuvuta maji, mawe, kokoto, mifuko ya saruji, mchanga na hundi katika kata za Bigwa, Mkundi na Mindu katika mfululizo wa kutekeleza ahadi za alizoahidi ikiwa ni mpango wa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) 2010.
Wananchi hao walisimamisha msafara wa mbunge huyu wakati akitokea katika kijiji cha Mjipya mtaa wa Vituli alikokwenda kupeleka mipira ya kuvuta maji rola mbili baada ya wakazi hao kuibua mradi wa maji ili kuondokana na kero ya kusaka maji kwa kutembea umbali mrefu.
Wakizumgumza mbele ya mbunge huyu walisema kuwa mtaa huyo wa Mwanzamgumu unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu mibovu ya barabara, kero ya tozo ya huduma ya maji ya sh100 na kutokuwepo kituo cha polisi kutokana na mtaa huo kuwa na mkusanyiko wa wafanyabiashara mbalimbali wanaofika eneo hilo kununua matunda aina mbalimbali.
Shani Malewela alisema kuwa Mwanzomgumu kumekuwa na kero nyingi lakini kero hizo zinazidiana ikiwemo ya kutozwa tozo ya kuchangia huduma ya maji sh100 ambayo imekuwa kubwa kwao kwani imekuwa ikiwalamizi kutumia zaidi ya sh500 kwa siku ili kukidhi mahitaji ya maji katika matumizi ya ndani ya nyumba.
Zaina Salmu na Matrida Msuva walisema kuwa kutokana na mtaa huo kukusanya wafanyabiashara wanaofika kununua ndizi na matunda mengine ipo haja kwa serikali kujenga kituo cha polisi na kuboresha miundomimbunu ya barabara eneo hilo limekuwa likojitokeza matukio ya mbalimbali ya kihalifu likimo la mwaka jana majambazi kupora pesa za wafanyabiashara kabla ya kujeruhi kwa risasi na kuua. Walisema kwa mbunge huyu.
Akijibu hoja za wananchi hao, mbunge wa jimbo hilo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood alisema kuwa baada ya kero ana uwezo wa kuzishughulikia ikiwemo ya ujenzi wa kuchangia kwa kuchangia matofali na vifaa vingine na kusaidia upatikanaji wa vifaa kwa ajili ya kuboresha miundomimbu ya barabara.
Abood alisema kuwa suala la tozo ya kuchangia huduma ya maji ya sh100 kwa kila ndoo na kudai hilo hapaswi kuliingilia kwani ana imani limepitishwa katika vikao halali vya serikali ya mtaa huyo wa Mwanzomgumu.
“Jamani mimi natoka kule Vituli ambako wenzenu wameibua mradi ya majisafi na majisalama, hapa mnaponiona, sasa nyinyi mnasema mnatozwa ndoo sh100 katika bomba la serikali ya mtaa wenu, kwa hilo siwezi kusema chochote ila naomba mmniitie viongozi wenu wa serikali ya mtaa ili tujadili pamoja ili lile linalowezekana kufanywa na ngazi ya juu niwasilishe halmashauri na lile ambalo tuna ubavu wa kulifanya wenyewe tulifanye”. Alisema Abood.
Viongozi hao wa serikali ya mtaa baada ya kuitwa na mbunge huyu ili kuweza kusikiliza kero za wananchi hao pamoja waligoma kufika eneo huku wakimtaka mbunge huyo kwenda walikokuwa wamekaa viongozi hao jambo ambalo mbunge huyo naye alishindwa kwenda kutokana na kubwana na ratiba ya ziara katika kata tatu za Bigwa, Mindu na Mkundi.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / WANANCHI WAWASHTAKI VIONGOZI WA SERIKALI YA MTAA KWA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment