BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATANO WAHIFIA KUFARIKI DUNIA KATIKA MLIPUKO MTAA WA PANGANI MJINI NAIROBI.

 
WATU kadhaa wamehofiwa kufariki kufuatia mlipuko uliotokea ndani ya gari moja dogo la abiria katika mtaa wa Pangani mjini Nairobi.



Duru zinaarifu kuwa karibu watu 5 huenda wamefriki katika shambulizi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu 15 waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini. 


Hata hivyo polisi hawajatangaza idadi rasmi ya watu waliojeruhiwa wala wale waliofariki. 


Mlipuko huo umesemekana kutokea ndani ya matatu iliyokuwa inakwenda katika mtaa wa Eastleigh ambao una idadi kubwa ya wasomali wanaoishi huko.


Athari za mlipuko huo hazikuyasaza magari mengine manne yaliyokuwa karibu na matatu hiyo.


Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliokusanyika katika eneo la shambulizi kujionea yaliyokuwa yanajiri.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: