Diwani wa kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro, Ally Kalungwana akiwa na kapu akitembeza kuchangisha fedha wakati wa harambee ya ununuzi wa madawani na ujenzi wa tundu la choo ya shule ya awali ya Baraka Baptisti Mwembesongo ambapo jumla ya sh62,000 zilipztikana huku ikihitajika kiasi cha sh850,000 kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo katika mahafali yaliyofanyika mtaa wa Sadani katika kata hiyo mkoani Morogoro. PICHA/MTANDA BLOG
Na Mtanda Blog, Morogoro.
DIWANI wa kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro, Ally Kalungwana ametoa wito kwa wazazi kuwa na tabia ya kuwapeleka watoto kujiunga na elimu ya awali kwani itawasaidia watoto kuanza kukabiliana mapema na changamoto za elimu huku ikitoa mwanga bora katika masomo ya shule ya msingi.
Akizungumza wakati wa mahafali ya shule ya awali ya Baraka Baptisti Mwembesongo mjini hapa, Kalungwana alisema kuwa njia pekee ya kuondokana na baadhi ya wanafunzi kutojua kusoma na kuandika katika shule za msingi na sekondari ni lazima wazazi kuiunga mkono serikali kwa kujenga tabia ya kuwapeleka watoto mapema kujiunga na elimu ya awali hiyo itawasaidia kuanza kukabiliana mapema na changamoto za elimu.
Kalungwana alisema kuwa faida kubwa kwa kumwanzisha mtoto elimu ya awali ni kupata ufahamu mapema pindi anapojiunga na masomo ya shule ya msingi kutambua changamoto za elimu kuanzia elimu ya awali, msingi na sekondari huku ikirahisisha kazi ya ufundishaji kwa wanafunzi ambao wameptia elimu ya awali.
“Zamani shule za awali zilikuwa chache sana na walimu walikuwa na kazi kubwa sana ya kufundisha lakini sasa hivi shule za awali zipo nyingi mno, jamani wazani hebu tubadilike kwa kuwapeleka watoto mapema katika shule za awali wapate elimu mapema na hii itasaidia sana kufuta kabisa tatizo la wanafunzi kutojua kusoma kwa shule za msingi na sekondari”. Alisema Kalungwana.
Naye mwalimu mkuu wa shule ya awali ya Baraka Baptisti Mwembesongo, Samwel Chiluwa alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na madawati kabisa kwa wanafunzi kukaa katika benchi huku wakihitaji kupata tundu nyingine la choo baada ya lililopo kukidhi mahitaji kutokana na uwingi wa wanafunzi.
Chiluwa alisema kuwa kuna uhitaji wa madawati 60 na kuongezewa tundu la choo moja kufanya idadi ya matundu kuwa mawili ili kuendana na uwingi wa wanafunzi huku akieleza kuwa wazazi wamekuwa wakirudi nyuma katika suala la ulipaji wa ada ambao ungesaidia kupunguza baadhi ya changamoto na watoto kusoma katika kaa katika benchi.
Tayari watoto 41 wamehitimu elimu ya awali ambao watajiunga na shule za msingi mwaka wa masomo wa 2014 huku Diwani wa kata hiyo akitaka watoto wote kujiunga na shule za msingi zilizopo katika kata hiyo huku akitoa zawadi ya vitabu vya soma kwa hatua kwa kila mwanafunzi waliohitimu na wale wanaobakia ikiwemo kalamu na vichongeo.
0 comments:
Post a Comment