MZEE MANDELA NA MWANAMUZI WHITNEY HOUSTON KULIA MJINI PRETORIA MWAKA 1994.
MANDELA alifanya mengi na kusema mengi. Hata hivyo kuna kauli yake moja ambayo inaweza kuchukuliwa kama alikuwa anaiaga dunia.
MANDELA alifanya mengi na kusema mengi. Hata hivyo kuna kauli yake moja ambayo inaweza kuchukuliwa kama alikuwa anaiaga dunia.
Katika mkanda wa historia yake, “Mandela: The son
of Africa, father of a nation, uliorekodiwa miaka kadhaa baada ya
kustaafu kwake urais wa Afrika Kusini, anasema:
“Kifo ni kitu ambacho kipo karibu na hakiepukiki,
pale mwanadamu anapomaliza kufanya kazi aliyotakiwa kuitekeleza kwa
ajili ya watu wake na nchi yake. Anaweza kupumzika kwa amani, naamini
nimefanya kile nilichopaswa kukifanya, na hiyo ndiyo maana nitalala kwa
maisha ya milele.”
Katika mkanda huo ameeleza maisha yake kwa urefu,
hatua kwa hatua na katika makala haya, tutaeleza simulizi ya mambo
yaliyomkuta baada ya kutoka gerezani alikokaa kwa miaka 27, hadi kuwa
rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.
“Nilipotoka jela, niliona ilikuwa ni nafasi nzuri
ya kukaa na mke wangu, nilimwambia kuwa sasa nipo tayari kuendeleza
familia yetu,” Mandela anasema katika mkanda wa historia yake.
Hata hivyo ndoto hiyo ya Mandela haikufikiwa kwani mwezi mmoja tu tangu alipoachiwa, mkewe Winnie alikamatwa na polisi.
Winnie alishikwa kwa kosa la unyanyasaji, kuteka na kumuua Stompie Moeketsie, kijana ambaye alikuwa mwanaharakati wa ANC.
Kijana huyo alipotea na baada ya muda alikutwa amekufa.
George Bizos ambaye ni mwanasheria wa familia
hiyo, anasema kuwa Mandela hakuamini kuwa Winnie amefanya kosa hilo, na
hivyo alisimama naye kuhakikisha anamsaidia.
Mwaka 1992 Winnie alionekana hana kosa la mauaji, alibaki na kosa moja tu la kuteka.
Kadri kesi hiyo ilivyoendelea, ilikuja kuonekana kuwa Winnie hakuwa na kosa lolote na hivyo kuachiwa huru.
Akizungumza nje ya mahakama baada ya kuachiwa
huru, Winnie anasema kuwa, “Hata kwenye mahakama zao wenyewe tumeonekana
hatuna hatia.” MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment