BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK SLAA AMTAKA MKAGUZI NA MDHIBITI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUMFANYA KUFANYA UKAGUZI OFISI ZA SPIKA WA BUNGE NA WABUNGE SAFARI ZOTE ZA NJE YA NCHI.

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbroad Slaa, ameibukia suala la matumizi mabaya ya fedha unaofanywa na wabunge na kutaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi safari zote za nje zinazofanywa na wabunge pamoja na ofisi ya Spika.



Akizungumza na mamia ya wananchi wa kijiji cha Kigwa wilaya ya Uyui jimbo la Igalula mkoani Tabora, alisema Bunge limegeuka kuwa sehemu ya kuhujumu fedha za Watanzania.



"Bunge limegeuka sehemu ya kupigana majungu, kufanya siasa ndani ya bunge, mbunge akiugua hata mafua anapelekwa nje ya nchi kutibiwa," alisema.



Dk. Slaa alisema kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma ndani ya Bunge, Watanzania waunganishe nguvu zao kupiga kelele ili bunge lirudi katika mstari wake wa kutetea wananchi kupata maendeleo.



Alisema amepata barua kutoka ofisi ya Bunge ambayo inaonyesha kuwa kati ya Julai-Oktoba Bunge limeomba Sh. bilioni 23.



"Shilingi bilioni 23 zilizoombwa na Bunge ambazo wanagawana tu zinaweza kujenga madarasa 300 ya shule, madarasa 300 yanatumika kwa ajili ya kupigana majungu,bunge limeacha misingi yake ya kutetea wananchi," alisema.



Alisema katika barua hiyo iliyosainiwa na Katibu wa Bunge, Dk. Kashilila, imetoa mchanganuo kuwa Sh. bilioni 2.890 zimetengwa kwa ajili ya posho za jimbo kwa wabunge.



Sh. bilioni 2.218 zimetengwa kutumika katika vikao vya kamati za bunge ambavyo hazina manufaa yeyote kwa wananchi na gharama za kamati teule za uchunguzi zimetengwa milioni 300.



Dk. Slaa alisema barua hiyo inaonyesha kuwa gharama za wabunge kwenda nje ya nchi zimetengwa Sh.bilioni 1.2, safari za viongozi nje ya nchi, Spika na Naibu Spika zimetengwa Sh.milioni 300.



"Wabunge wanatengewa fedha kwenda kutalii Ulaya katika nchi maskini kama Tanzania, ni lini wamerudi na kuleta tija kwa wananchi,mbunge anapata takribani milioni 9 kwa ajili ya kutembelea wananchi wake lakini bado wapo ambao hawaendi,"alisema.



Aliongeza kuwa matibabu ya wabunge nje ya nchi zimetengwa Sh.milioni 300 na gharama za uendeshaji wa ofisi ya Bunge ni Sh.bilioni moja.



Dk. Slaa alisema wakati fedha hizo za kuanzia Julai hadi Oktoba zikiendelea kutafunwa, ofisi ya Bunge kwa mara nyingine imeomba fedha nyingine Sh. Bilioni 29 kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu, Alisema kutokana na hali hiyo ni takribani Sh. bilioni 52 zimeombwa na ofisi ya Bunge na kwamba ni wakati sasa kwa CAG kufanya ukaguzi wote wa wabunge na ofisi ya Bunge. 

CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: