RAIS
Jakaya Kikwete amebariki maamuzi ya wabunge na kutengua nyadhifa za
mawaziri wanne wa Baraza la Mawaziri kufuatia kashfa ya Operesheni
Tokomeza Majangili na Operesheni Kimbunga.
Hii ni mara ya tatu kwa Baraza la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete
kujiuzulu kufuatia kashfa mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2008 –
2013.
Uamuzi wa kujiuzulu kwa mawaziri hao ulitangazwa jana Bungeni na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili na
Utalii, kusimama bungeni na kutangaza mwenyewe kujiuzulu na kufuatiliwa
na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. David Mathayo, ambaye
pamoja na kutakiwa na wabunge ajiuzulu, aligoma kutangaza uamuzi huo.
Rais Kikwete alitoa uamuzi huo akiwa nchini Marekani kwa matibabu baada
ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kumpelekea maoni yaliyotolewa na wabunge.
Waliowajibishwa ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo
David, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki , Waziri
wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Shamsi Vuai
Nahodha.
Hata hivyo, Dk. Nchimbi na Waziri wa Ulinzi, Nahodha, hawakuwepo ukumbini , wakati uamuzi huo ukitolewa.
Hatua ya Rais ilitangazwa jana saa 2:30 usiku bungeni na Waziri Mkuu
Pinda , aliyekuwa anatoa msimamo wa serikali kuhusiana na hoja hiyo ya
kuwawajibisha kutokana na uovu uliofanywa na watekelezaji wa
operesheni hiyo uliosababisha mauaji ya watu 19.
Waziri Mkuu ambaye naye alitakiwa na wabunge kujiuzulu hakuwa tayari kujizungumzia wala kujibu hoja zilizomtuhumu.
Alisisitiza kuwa operesheni hiyo imesimamiwa na wizara tatu za
Maliasili na Utalii, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mambo ya Ndani
hivyo awali alizungumza na mawaziri wote wanne na kukubalina kuwa
katika mazingira hayo na kauli za wabunge walizoshauri wachukulie kwa
msingi kuwa ni busara wakubali ushauri wa Bunge wakukubali kuwajibika.
“Waheshimiwa wote wanne wamekubali kujiuzulu na kilichofanya
walikubali kufanya hivyo ni kwamba vyombo vilivyohusika viko chini ya
usimamizi wao.”
DK. MATHAYO
Akizungumzia Dk. Mathayo alisema kwa maana ya operesheni tokomeza ni
vigumu kusema kuwa alihusika moja kwa moja kwani hakuwa na vyombo
vilivyosimamia operesheni hiyo na kwamba hakuhusika na vitendo
vilivyojitokeza .
Lakini kwa msingi huo alitakiwa kujiuzulu kwa kuwa
anasimamia Wizara ya Mifugo na ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa
alishindwa kusimamia mifugo ambayo imeingia kwenye hifadhi.
“Nilimueleza kuhusu Mathayo kuwa anaweza asihusike moja kwa moja na
operesheni tokomeza lakini pengine aangaliwe kama yeye ni msimamizi wa
mifugo. Hii inaweza kuchukuliwa kuwa ndiyo maana ameshindwa kusimamia
mifugo inayoingia kwenye hifadhi za taifa”.
Alichosema hapana ni kwamba hakuna haja ya kugombana kwenye jambo hilo
ambalo ni kubwa hivyo si vibaya na yeye akaliona kwa mtizamo huo na
kujiuzulu kama wengine.
TUME
Akizungumzia kuhusu kuundwa kwa tume aliongea na Rais na hilo ameliunga
mkono na kushauri tume iundwe na matokeo yake yapatikane kwa muda
mfupi ili watendaji wote waliohusika bila kujali ni wa ngazi gani au
taasisi gani wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu.
RIPOTI
Akiizungumzia matukio yaliyoibuliwa na kamati hiyo ya unyanyasaji,
udhalilishaji na mauaji ya watu na mifugo haukubaliki na serikali
itachukua hatua . Na kusisitiza kuwa kikwazo kikubwa ni namna
operesheni iliyotekelezwa na kusimamiwa.
Aliwataka mawaziri hao waone kuwa ni sehemu ya jukumu lao na
anakubaliana na wabunge wanaotaka mawaziri wabebe lawama kwa hiari yao
wenyewe.
Nimejaribu kutizama maelezo yaliyotolewa taarifa hizo zinahitaji
kuthibitishwa zaidi. Ushauri wa Mwanasheria umezingatia zitakuwepo hatua
za kiutawala na za kisheria.
Kuna uvunjifu mkubwa wa sheria na kunahitajika tume ya kimahakama
kuwachunguza ili wahusika washughulikiwe, naamini muda mfupi kadri ya
mwezi mmoja tupate taarifa ya uchunguzi na hatua kwa kila mmoja
zichukuliwe.
Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa kutunza mali asili hasa wanyama pori
akieleza kuwa sensa inaonyesha kuwa katika hifadhi ya Selous kulikuwa
na 55,000 lakini sawa wamebakia tembo 13,000.
WAZIRI KAGASHEKI AIBUKA SHUJAA
Akitoa maelezo ya kujiuzulu bungeni Balozi Kagasheki alisema “mimi ni
mtu mzima nimesikia hisia na sauti za wabunge na mimi nasema ..
Mheshimwa Rais Dk. Jakaya Kikwete, aliponiteua ilikuwa ni katika furaha
yake naamini kabisa aliniamini kuwa ningeweza kufanya kazi kama
alivyotegemea”
“Lakini kutokana na operesheni hii kuna mabaya yametokea naamini
uchunguzi utafanyika kuwafahamu waliohusika….niombe tu nimeseme kuwa
mimi mwenyewe nimewasikia kwa kauli yangu natamka wazi kuwa ni nia
yangu kushuka ngazi hii ya uwaziri, ninajiuzulu.”
Alisema na kushangiliwa na Bunge na kuahidi kuwa atachukua hatua ya kuzitaarifu mamlaka zilizompa jukumu hilo.
Mathayo ‘ ninaonewa’
Alilalamika kuwa anahukumiwa kuwa mtuhumiwa bila kuhojiwa. Alisema
ripoti nzima haikutaja kuwa amehusika na operesheni tokomeza na kuongeza
kuwa hakuitwa kuhojiwa na kamati na kwamba hajawahi kuona mahakama
inayomhukumu mshitakiwa bila kumhoji.
Alisisitiza kuwa ameonewa na Mungu mwenyewe atawashughulikia hao wanaotaka ang’oke na kwamba alikuwa anasali zaburi ya 72.
Aliiponda ripoti hiyo ya kamati kwa kutoa taarifa za uongo kuwa
Tanzania ni nchi ya pili kwa mifugo lakini haina sera na mipango ya
muda mrefu ya kuendeleza mifugo. Alisema sera ipo na ilipitishwa na
Bunge mwaka 2006 na pia kuna mipango ya muda mrefu na mfupi ya
kuendeleza mifugo.
“Kwangu haingii akilini mimi kuambiwa sina sera sina mipango , alisema
na kujitetea kuwa matatizo ya sekta ya mifugo ni ya kitaasisi”. CHANZO:
NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment