BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PROFESA MUHONGO NI MTU MWENYE HULKA YA KUSEMA UONGO, NI VITA YA MANENO KATI YAKE NA REGINALD MENGI KATIKA ISHU YA GESI.

mengi
REGINALD MENGI.


DAR ES SALAAM.
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema kauli zinazotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo dhidi yake kuhusu uwekezaji katika sekta ya gesi nchini hazina ukweli wowote.

Prof. Sospeter Muhongo.

Mengi jana alitoa taarifa yake katika vyombo vya habari na kueleza kuwa waziri huyo ni mtu mwenye hulka ya kusema uongo, kauli ambayo ameitoa ikiwa zimepita siku mbili tangu waziri huyo kudai kuwa Mengi anamiliki vitalu vingi vya gesi, kwamba anataka kupewa upendeleo wa kupewa wakati hawezi kuviendeleza.


Huku akitaja mambo kadhaa ya uongo kuhusu waziri huyo, Mengi alisema,“Sikutegemea kama Muhongo ataendeleza vita dhidi yangu. Mtu huyu ana hulka ya kusema uongo, amewahi kuwaahidi Watanzania kuwa hakutakuwa na mgawo wa umeme, lakini upo mpaka sasa.”


Alisema hamiliki migodi mingi ya madini kama inavyodaiwa “Ukweli ni kwamba, mimi namiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba.”


Alifafanua, “Muhongo anafahamu kwamba kuna aina sita za leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini.


Lakini kwa makusudi kabisa anafananisha leseni ya Mtanzania anayetafuta au kuchimba kokoto na leseni ya mwekezaji wa kigeni anayetafuta au kuchimba urani au dhahabu. Kweli unaweza kufananisha kokoto na dhahabu.”


Alisema kuwa licha ya kuwa utafutaji wa madini ndiyo husababisha watu kugundua eneo lenye madini, kuanzia Julai mwaka jana Waziri Muhongo amepandisha tozo za vitalu kwa asilimia kati ya 100 na 500 na kusababisha Watanzania wengi kurudisha leseni zao. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: