MARAa tu baada ya kupokea habari juu ya kifo cha Madiba Alhamis jioni,
rais wa Marekani Barack Obama alitoa hotuba na rambi rambi zake akisema
Mandela aliishi na kuifanya ndoto yake kutimia ya kuwa na Afrika Kusini
huru na yenye demokrasia.
Rais Obama alikwenda kwenye chumba cha White House anakozungumza na
waandishi habari wa Ikulu mara tu baada ya kupokea taarifa za kifo cha
Mandela zilizotangazwa na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Obama alisema marehemu Mandela katika uhai wake aliishi kwa kupigania
ndoto yake na akaitimiza. Alifanikiwa katika mambo mengi kuliko
inavyotegemewa kwa mtu yeyote. Leo hii amekwenda nyumbani.
umempoteza mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa, mtu jasiri, binadamu
mzuri ambaye tumeishi naye dunia hii. Wasifu wake utadumu milele.”
Rais Obama pia aliamrisha bendera zote za Marekani zipepee nusu mlingoti hadi Jumatatu jioni.
Viongozi wengine wa dunia wanamkumbuka mpiganaji dhidi ya ubaguzi wa
rangi na rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela. Marais wa
zamani wa Marekani Jimmy Carter, Bill Clinton, George W. Bush na George
H.W. Bush pia walimsifia bwana Mandela kama kinara wa uhuru, utu na
mwanaharakati wa kutetea usawa.
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -Moon amesema amesikitishwa
sana na kifo chake na ametoa mwito kwa watu kufuata nyayo za mzee
Mandela. Mkuu wa tume ya Jumuiya ya Ulaya Jose Manuel Barosso alisema Bw
Mandela alibadilisha historia ya dunia wakati waziri mkuu wa Israel
Benjamin Netanyahu akisema marehemu Mandela alikuwa mtu mwenye maono
aliyepinga ghasia.
Na huko Afrika Kusini umati mkubwa wa watu umekusanyika nje ya nyumba ya
Bw. Mandela mjini Johanesburg kuimba na kucheza, kutoa heshima zao za
mwisho wakifuata utamaduni wa Afrika Kusini baada ya kifo chake.
0 comments:
Post a Comment