BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIONGOZI WA TANZANIA KUNA JAMBO WANAPASWA KUJIFUNZA KUTOKA KWA MZEE MANDELA NA NYERERE.



MZEE MABDELA AKIFURAHIA JAMBO NA WAJUKUU ZAKE HUKU WATOTO HAO  WAKIONAKANA KUTOKUWA PAMOJA KATIKA KICHEKO HICHO WAKATI WA UHAI WAKE.

Mzee Mandela.
 
Na MTANDA BLOG, Morogoro.
VIONGOZI wa Tanzania kuna jambo moja ama zaidi ya hilo wanapaswa kujifunza kutoka kwa Mzee Nelson Mandela akiwemo na Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania, Mzee Julius Nyerere kutokana na matendo yao enzi za uongozi wao.


Moja ya mambo ambayo wanapaswa kujifunzi ni uongozi bora uliojaa hekima, busara n:k lakini kikubwa ninachoona ni viongozi wetu kujifunza viongozi hao namna walivyotumikia nchi kwa nyakati tofauti na hawakuwa na tamaa ya kung'ang'ania madaraka kama marais wa nchi nyingine za afrika na dunia kwa jumla ikiwemo na baadhi wa viongozi ndani ya serikali ya Tanzania.
MWALIMU JULIUS NYERERE.

Ifikie wakati viongozi wenye wawe na tabia ya kushiba madaraka na kuachia ngazi kupisha vijana nao kuendesha kurudumu kwani kwa kuiga mfano wa viongozi hao kutajenga dhana ya kuwaamini wale wanaoweza kuchukua majukumu yao.

Tumeshuhudia baadhi ya vyama vya siasa viongozi wa juu kung'ang'ania kuendelea kushikilia madaraka ilhali wapo vijana ambao wana uwezo wa kushika nyadhifa hizo na kufanya vizuri wao wakiwa waongozaji pindi wanapoona wanaenda ndivyo sivyo.

Mandela kama kinara wa uhuru, utu na mwanaharakati wa kutetea usawa sifa hiyo huwezi kamwe kumwelezea Mwalimu Julius Nyerere ambaye ni kama wanafanana kitabia japo wamekuwa na matukio tofauti tofauti wakati wakisaka uhuru wa nchi zao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: