Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini,Nelson Mandela.
CAPE TOWN.
BARAZA la Jiji la Cape Town, limeidhinisha matumizi ya Rand72 milioni (Sh12.2 bilioni) kwa ajili ya mazishi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Taarifa ya baraza hilo iliyotolewa jana ilisema
bajeti hiyo ilipitishwa katika kikao cha dharura na kwamba itasaidia
kufanikisha shughuli zote za maandalizi ya kumuaga Mandela katika mji
huo.
Mbali na kupitisha bajeti hiyo, pia liliamua
kuweka usafiri wa bure kwa kutumia treni za mji huo – MyCiTi na mabasi
marefu ya Golden Arrow kuwafikisha watu katika maeneo maalumu
yaliyotengwa kwa ajili ya kuonyeshwa shughuli za kuaga mwili.
Meya wa mji huo, Patricia de Lille alisema
wameandaa pia mkakati maalumu kwa watu watakaokuwa wanatembea kwa miguu
ili kushiriki katika tukio hilo muhimu na la kihistoria nchini humo.
Alisema taratibu za kuaga zitafanyika kesho na
kwamba zitaendeshwa kwa utaratibu maalumu na wa kipekee kwa sababu mji
huo una historia ya kipekee kwa kiongozi huyo aliyejitoa kudai uhuru.
“Kwa aibu yetu, mji huu ndimo lilimo gereza ambalo alitumikia kifungo cha miaka karibu yote 27,” alisema Lille na kuongeza:
“Lakini pia hapa ndipo alipotolea hutuba yake ya kwanza mara baada ya kuachiwa na kutaka iandikwe katiba mpya.”
“Kwa zawadi hii, tumemfanya Madiba kama sehemu
inayoishi milele katika Serikali na jiji hili. Madiba amechangia mengi
ambayo hapa tunajivunia leo hii. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment