BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ULINZI WAIMARISHA KATIKA TUKIO LA KUAGA MWILI WA MZEE NELSON MADIBA MANDELA JOHANNESBURG LEO.

 
MSEMAJI WA POLISI AFRIKA YA KUSINI LUTENI JENERALI, SOLOMON MAKGALE.


LEO ni siku ya kitaifa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.



Polisi wamejiandaa kutoa ulinzi mkali, ambao haujapata kutokea nchini hapa. Shughuli hiyo inafanyika katika uwanja wa mpira wa Soweto, ujulikanao kama FNB.


Katika kuimarisha ulinzi, maelfu ya askari Polisi watamwagwa mitaani katika maeneo yote yanayohusika, kuhakikisha shughuli hiyo inafanyika kwa usalama wa hali ya juu.


Mamlaka za kipolisi zimesisitiza jana kuwa iwapo umati wa wanaotaka kushiriki mazishi hayo, utakuwa ni mkubwa zaidi, hawatakuwa na njia nyingine, bali kuzuia watu wasifike zaidi katika eneo hilo ili kuepuka madhara zaidi.


Waombolezaji wakiwemo viongozi wa mataifa mbalimbali, wanatarajiwa kufurika katika uwanja huo wa mpira wa Soweto, kumuaga kiongozi huyo kinara wa kupinga siasa za ubaguzi wa rangi. Uwanja huo una uwezo wa kubeba watu 95,000.


Mandela alionekana hadharani kwa mara ya mwisho katika uwanja huo, wakati wa kilele cha mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2010 wakati huo uwanja huo, ukijulikana kama Soccer City.


Luteni Jenerali Solomon Makgale, ambaye ni Msemaji wa Polisi alisema askari wengi watakuwa na kazi za kuwaelekeza waombolezaji na kuwalinda waandamanaji, ambao wataenda kwenye uwanja huo.


“Tutakuwa makini kuhakikisha watu wanatoa heshima za mwisho katika mazingira ya amani,” alisema Kamanda Makgale wakati akizungumza na Shirika la Habari la Associated Press.


Makgale alisema katika shughuli zinazohusu maziko ya Mandela, Polisi wanafanya kazi kwa karibu na Idara ya Usalama pamoja na wanadiplomasia, ili kuhakikisha wageni kutoka nje ya nchi wanawekewa utaratibu mzuri.


Maandalizi FNB Jana wafanyakazi walikata vioo vya mbele vilivyoko katika uwanja huo wa FNB na waliweka vioo vya kuzuia risasi katika eneo, ambako watafikia viongozi mbalimbali kwa ajili ya kuwalinda viongozi hao wa kigeni.


Miongoni mwa wageni hao watakaofika katika shughuli hiyo ya kitafa ni Rais wa Marekani, Barack Obama ambaye anatarajia kupewa fursa ya kuzungumza na waombolezaji.
Usalama.


Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Collins Chabane jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa maofisa wa Serikali, hawapaswi kubashiri umati utakaofurika leo, bali wabashiri usalama wa umati huo.


“Pale tutakapoona idadi ya watu ni kubwa zaidi, ni lazima tuzuie watu kuingia,” alisema Chabane.


Mandela alifariki Alhamisi akiwa na umri wa 95. Baada ya shughuli ya leo uwanjani hapo, kesho Jumatano mwili wa Mandela utapelekwa katika majengo ya Serikali ya Muungano katika mji wa Pretoria, ambako utakaa hadi siku ya Ijumaa. HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: