BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIFO CHA MZEE NELSON MANDELA, AFRIKA YA KUSINI YAPATA PIGO.


RAIS wa kwanza wa Afrika Kusini na mpinga siasa za ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela amefariki nchini humo akiwa na umri wa miaka 95.


Taarifa za kifo chake zimetangazwa na rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma ambaye amesema Mandela amefariki majira ya saa 2.50 usiku wa Alhamisi kwa saa za Afrika Kusini.

Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwenye mapafu kwa muda mrefu, alilazwa na baadaye kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwake mjini Pretoria.
Tayari viongozi mbalimbali duaniani wameshaanza kutuma salamu za rambirambi kwa familia na taifa la Afrika Kusini.

Viongozi hao ni pamoja na Rais Barack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: