Mwenyekiti wa klabu ya Morogoro Veteran na Meneja wa tawi la benki ya NMB Masika Morogoro, Hamis Madole.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mjini hapa kwa niaba ya wachezaji wenzake aisema kuwa shahada ya pili aliyotunukiwa katika chuo kikuu cha Mzumbe anapaswa kuongeza juhudi hasa katika utendaji kazi na kuleta ubunifu kutokana na elimu hiyo.
Mwenyekiti wa klabu ya Morogoro Veteran na Meneja wa tawi la benki ya NMB Masika Morogoro, Hamis Madole akifurahia jambo na washambuliaji zamani wa klabu ya Pamba ya Mwanza, Mtibwa Sugar na Moro United, Ally Bushiri kushoto na Boniface Mapunda aliyewahi kuichezea klabu ya daraja la pili ya SUA kulia wakati wa hafla ya kumpongeza baada ya kuhitimu shahada ya pili ya corporate managenment (MBA) katika chuo kikuu cha Mzumbe kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Pamba, Mtibwa Sugar na Moro United Ally Bushiri alisema kuwa kiwango cha elimu alichonacho Mwenyekiti wao kwa sasa kinampa wiko wa kubuni mambo mapya hasa ukizingatia wakati huu wa ushindani mkubwa wa kibiashara hususani taasisi anayofanyia kazi.
Bushiri alisema kuwa Mbona (Hamis Madole) ameongeza shahada ya pili na taasisi ambayo anafanyia kazi benki ya NMB ina changamoto kubwa hasa kwa kusaka mbinu mpya za kuwashawishi wateja ili kuweka fedha zao katika benki hiyo ambayo inahitaji mbinu mbadala ya kubuni wazo la ushawishi na kuwa kutokana na ushindani mkubwa uliopo ndani ya taasisi hizo za fedha hapa nchini.
“Ukiniuliza vip nafasi ya upachikaji mabao katika klabu yetu ya Moro Veteran bila shaka kila mchezaji atakueleza kuwa jamaa anajua kucheka na nyavu japo katika ujana wake hakuweza kupata nafasi ya kuchezea klabu kubwa ila nina imani naye kubwa tu katika nafasi yake ya umeneja benki ya NMB Masika hivyo inabidi akaze buti ili apate mafanikio zaidi” alisema Bushiri.
Naye Mwenyekiti huyo, Hamis Madole (Mboma) alisema ushauri huyo ataufanyia kazi na kujitahidi kubuni mbinu mbadala zitakazo wezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo zile zinazoimbuka taasisi hiyo hiyo ya fedha kwa kusaka wateja kuweka fedha katika benki hiyo.
Katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa iliwakutanisha wachezaji wa zamani waliowahi kuwika akiwemo Ally Bushiri, Pamba, Mtiba Sugar na Moro United, Adam Seleman aliyetamba na Reli ya Morogoro na Simba SC, Seleman Shabaan (Sule Boy) akitamba na kikosi cha Moro United na Pan Afrika.
Wengine ni Mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake mkoa wa Morogoro, Edna Lema, Detha Thomas aliyekipiga klabu ya Polisi Moro SC, Ally Shomari Reli Morogoro na Polisi Moro SC, Omari Mkesi Reli Morogoro na Victa Bundara, Yanga Sport Club, Mtibwa Sugar na Polisi Moro.
0 comments:
Post a Comment