BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA: WAZIRI MKUU NAMNA ALIVYONOGESHA MAHAFALI YA CHUO KIKUU MZUMBE MOROGORO, MENEJA NMB ATUNUKIWA SHAHADA YA PILI, MTOTO WAKE AHITIMU SHAHADA YA UZAMILI YA UONGOZI KATIKA MIFUMO YA AFYA.

Waziri mkuu Mizengo Kayanda Pindaa (katikati) akizungumza wakati akiongea na Kingunge Ngombalemwile kulia na mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera mara baada ya Waziri kuhudhuria mahafali ya chuo kikuu cha Mzumbe kilichopo wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro. PHTO/MTANDA BLOG.

Mwenyekiti wa klabu ya Morogoro Veteran na Meneja wa tawi la benki ya NMB Masika Morogoro, Hamis Madole akipongezwa kwa kuvalishwa taji na kiungo mkabaji wa zamani wa klabu ya Pan Afrika na Moro United, Seleman Shabaan wakati mwenyekiti huyu alipopata shahada ya pili ya corporate managenment (MBA) baada ya kuhitimu katika chuo kikuu cha Mzumbe kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro jana.PHOTO/MTANDA BLOG.
Mwenyekiti wa klabu ya Morogoro Veteran na Meneja wa tawi la benki ya NMB Masika Morogoro, Hamis Madole akifurahia jambo na washambuliaji zamani wa klabu ya Pamba ya Mwanza, Mtibwa Sugar na Moro United, Ally Bushiri kushoto na Boniface Mapunda aliyewahi kuichezea klabu ya daraja la pili ya SUA kulia wakati wa hafla ya kumpongeza baada ya kuhitimu shahada ya pili ya corporate managenment (MBA) katika chuo kikuu cha Mzumbe kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro jana.PHOTO/MTANDA BLOG.
 
Mwenyekiti wa klabu ya Morogoro Veteran na Meneja wa tawi la benki ya NMB Masika Morogoro, Hamis Madole akicheza muziki na mkewe Mwanaisha Shomari wakati wa hafla ya kumpongeza baada ya kuhitimu shahada ya pili ya corporate managenment (MBA) katika chuo kikuu cha Mzumbe kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro jana. PHOTO/MTANDA BLOG.
 PG4A7887
Mtoto wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Janet Pinda  (kulia) akipongezwa na wadogozake, Nasirika  Nyema (wapili kulia) na  Namsi Pinda (kushoto) baada ya kutunukiwa  Shahada ya Uzamili  ya Uongozi  katika Mifumo ya Afya kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro, Desemba 6, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). PG4A7892
Mtoto wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Janet Pinda (Kulia)  akipongezwa na mdogo wake Nasirika Nyema baada ya kutunukiwa  Shahada ya Uzamili  ya Uongozi katika Mifumo ya Afya  kwenye Mahafali  ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mjini Morogoro Desemba 6, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: