TASWIRA YA RAIS JAKAYA KIKWETE NA MHE EDWARD NYOYAI LOWASSA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU MWAKA 2013 UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM.
UMOJA WETU NDIO NGAO YETU, UMOJA WETU NDIO ALAMA YA USHINDI TANGU 1961-2013.(MIAKA 52 YA UHURU WETU)
BADO SISI NI WAMOJA NA TUTAENDELEA KUWA WAMOJA KWA MASLAHI YA TAIFA NA VIZAZI VIJAVYO.
Kama taifa tuna kila sababu ya kujivunia Amani, Mshikamano, na Utulivu vitu ambavyo ni tunu pekee tuliyorithi kwa waasisi wa taifa letu.
Kwa sasa kila Mtanzania lazima awajibike na kutimiza wajibu wake ili Taifa lizidi kusonga mbele na kuwashinda maadui zetu Ujinga, Maradhi na Umasikini.
Kwa pamoja lazima tumuunge mkono Mh Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete katika jitihada zake mbali mbali za kuliletea taifa letu maendeleo makubwa na ustawi wa kijamii.
Na pia lazima tukiri kwa dhati toka moyoni kwamba Mh Rais ameitangaza vyema Tanzania katika medani ya kimataifa na kwa sasa tumepata heshima kubwa kama taifa na kuaminika katika uso wa kimataifa (Hongera sana Mh Rais)
Pia kama taifa lazima tuendelee kujivunia rasilimali watu tuliyonayo na tuitumie vyema katika kuleta manufaa kwa taifa na hasa nguvu kazi ya VIJANA WA TAIFA LETU.
BADO SISI NI WAMOJA NA TUTAENDELEA KUWA WAMOJA KWA MASLAHI YA TAIFA NA VIZAZI VIJAVYO. KUTOKA UKURASA WA MHE, Lowassa Ngoyai Edward
0 comments:
Post a Comment