BREMEN, UJERUMANI.
Bendi maarufu ya muziki wa
dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni, usiku tarehe 23
Novemba 2013 walifanikiwa kwa mara nyingine tena kuliteka jiji la Bremen,kule ujerumani.PICHA KWA HISANI YA NGOMA AFRICA.
Ngoma Africa Band walijikuta wapo katika kibarua kama kawaida yao
cha kushambulia kwa virungu vya muziki na kufanikiwa kuutapanua uwigo
wake kwa kuwanasa washabiki wengi wa kimataifa.
Bendi hiyo maarufu iliyojiimarisha na kujenga himaya ya kimataifa kwa kutumia muziki wake, imeshatajwa mara nyingi kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya, bendi
ya Ngoma Africa inafanananishwa sawa na kikosi maalumu cha kuzuwia
ghasia FFU, pia ina majina mengi ya utani na kiusanii kama vile viumbe
wa ajabu "Anunnaki Elien" n.k ambayo imepewa na washabiki au wapenzi
wake, kiongozi wake pia ana majina kama vile kamanda Ras Makunja wa
FFU, mtawala wa Anunnaki Empire.
0 comments:
Post a Comment