BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA KUTANDIKWA NA KLABU YA KCC MAPINDUZI CUP 2014 VISIWANI ZANZIBAR, SASA SIMBA SC KUIVAA MTIBWA SUGAR UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Asha Said.
MABINGWA wa Mtani Jembe na washindi wa pili wa michuano ya
Mapinduzi, Jumamosi watajitupa katika Uwanja wa Taifa, kuvaana
na timu ya Mtibwa Sugar.




Mchezo huo wa kirafiki utakuwa wa mwisho kwa klabu ya Simba,
kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, inayoanza kutimua
vumbi Januari 25 mwaka huu.



Akizungumza Dar es Salaam jana Kocha msaidizi wa Simba,
Suleiman Matola, alisema wameamua kupata mechi moja katika
uwanja wa taifa kabla ya kuanza kwa ligi.



Matola alisema sababu kuu ya kuamua kucheza mchezo huo ni
moja ya sehemu yao ya kuipa timu yao mazoezi katika uwanja wa
Taifa, ambao itachezea mechi zake za nyumbani.



Alisema wameamua kucheza mechi na timu ya Mtibwa, kwa
sababu wanaitambua bora wake, hivyo wakicheza nayo inawapa
maandalizi mazuri.



Matola alisema kuwa mchezo huo utafanyika majira ya saa 10.jioni,
ikiwa ni moja ya sehemu ya kocha wao Zdravko Lugarusic, kutaka
timu ngumu, ya kucheza na timu ya Simba.



"Haya ni maamuzi ya kocha mkuu Logarusic, anataka kuichezesha
timu yake na timu ngumu, ambayo itaipa mazoezi mazuri timu
yake, kabla ya kuanza kwaa ligi kuu"alisema Matola.



Simba iliyorejea juzi jijini Dar es Salaam, ikirtokea Zanzibar katika
michuano ya Mapinduzi, ambapo ilifika hatua ya fainali na kupata
ushindi wa pili wa michuano hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: