BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK JAKAYA NA DK BILAL WAWAJULIA HALI MAWAZIRI WAWILI HOSPITALI YA RUFAA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM

NI CLEOPA MSUYA NA HARUNA ALI SULEIMAN.
 Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo,  Salome Kassanga.
Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri Mkuu msaafu Mzee Cleopa David Msuya aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Januari 15 jijini Dar es Salaam. (Picha na Freddy Maro)
 Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa David Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo. Kushoto ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal. 
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Haruna Ali Suleiman, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo. Katikati ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Salome Kassanga. (Picha na OMR)
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: