Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freema Mbowe kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zubery Kabwe moja ya harakati za kukiendesha chama hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anapanga kumchukulia hatua za kisheria Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutokana na kile alichodai kuwa ni kuzusha tuhuma zenye lengo la kumchafua yeye binafsi na chama hicho.
Tuhuma hizo ni zile zilizowekwa katika mitandao
mbalimbali ya kijamii na kuandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari
kuanzia Januari 6 mwaka huu, zikimnukuu Zitto akieleza kuwa Mbowe
amewahi kuhongwa mamilioni ya fedha na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM),
Nimrod Mkono.
Tuhuma dhidi ya Mbowe ziliibuka baada ya
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumu Zitto kuwa amehongwa
magari mawili na Mkono.
0 comments:
Post a Comment