
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka amekifungia kwa muda usiojulika shughuli za uzalishaji, Kiwanada cha Sukari cha Mtibwa mpaka kiwanda hicho kitakapolipa madeni ya wafanyakazi na wakulima wa miwa.
Akitoa msimamo wa Serikali ya wilaya hiyo juu ya
kukifungia kiwanda hicho mbele ya wafanyakzi na wakulima hao katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za mtendaji wa kata ya
Mtibwa wilayani hapa, Mtaka alisema, wamechukua uamuzi huo baada ya
mabishano ya muda mrefu baina ya pande mbili kutofikia muafaka.
Mkuu huyo wa wilaya katika mabishano hayo ya muda
mrefu juu ya madai ya wakulima na wafanyakazi alisema wanakidai Kiwanda
cha Mtibwa zaidi ya Sh1.9 bilioni ambazo ni za mauzo ya miwa na
mishahara ya wafanyakazi.
Mtaka alisema shughuli nyingine kiwandani hapo
zitaendelea kama huduma ya afya, ulinzi na idara ya fedha ili kuwezesha
makundi hayo kupata mafao yao mwishoni mwa wiki hii kama ilivyoahidiwa
na uongozi wa kiwanda hicho.
Meneja mkuu Hamad Juma alisema, kiwanda hicho
kilikwama kulipa madeni hayo kutokana na uingizwaji mwingi wa sukari
nchini uliosababisha wao kukosa soko ingawa waliahidi kuanza kulipa
mwezi huu. LILIAN LUCAS
0 comments:
Post a Comment