ZAIDI ya wanafunzi 5,000 waliojiunga na kidato cha kwanza katika shule za
sekondari za serikali walibainika kutokujua kusoma na kuandika, hali hii
ilipigiwa kelele sana na serikali, wadau wa elimu na hata bunge
wakijiuliza swali kuwa walifauruje mitihani yao ya darasa la saba ?.Hata wabunge wakathubutu kusema kuwa Tanzania inatakiwa kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Guinnes (Guinnes Book of Record) kwa kufaurisha wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.
Sasa muhula wa kwanza kwa shule za sekondari ndio umeanza na wanafunzi wa kidato cha kwanza wameshaanza masomo.
Je Mwaka huu 2014 hali itakuwaje kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ?.

0 comments:
Post a Comment