DODOMA.
YAKIWA yamebaki masaa machache kabla ya Bunge Maalum la Katiba kuanza mjini hapa, Chama cha Mapinduzi kimesema kitaendelea kusisitiza mfumo wa serikali mbili kufuatia kikao cha siku mbili cha Halmashauri yake Kuu ya Taifa (NEC).
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipokutana na wanahabari kuzungumzia
changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika mfumo wa sasa wa kiserikali.
“Changamoto zote tumezitafakari [tukaona] jibu
lake sio serikali tatu,” alisisitiza Bw. Nnauye akiongeza “Bado sisi ni
waumini wa serikali mbili.”
Hata hivyo, msemaji huyo wa CCM alikiri kuwa ili
mfumo huu wa serikali mbili uendelee kufanya kazi, lazima baadhi ya
mambo yabadilike. “Sio serikali mbili kama zilivyo sasa,” alisema.
Bw. Nnauye anaamini NEC imejiandaa vyema
kuwasilisha hoja nzito zinazojibu maswali magumu kuhusu mapungufu ya
utaratibu wa sasa wa serikali mbili.
Hata hivyo, hakuwa tayari kuzitaja hoja hizo, akisema zitawekwa wazi wakati wa Bunge la Katiba.
Kusikiliza kauli rasmi tazama VIDEO.
0 comments:
Post a Comment