Makala baada ya kukagua tanki la maji katika mji mdogo wa Mvomero wilaya ya Mvomero.PICHA/MTANDA BLOG
Mkazi wa mji mdogo wa Lupiro akiwa amepumzika katika pikipiki huku akimsubiri mhudumu wa kisima kilichopo kijiji hicho ili kuweza kupata huduma hiyo wakati wa ujio wa naibu waziri wa maji Amos Makala wa kukakagua miradi ya maji wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.
Naibu waziri Amos Makala akizungumza jambo na wananchi wa kijiji cha Kibati juu ya miradi ya maji katika kijiji hicho kilichopo wilaya ya Mvomero.PICHA/MTANDA BLOG
Meneja wa kampuni ya Ruqman, Said Assey akimsikiliza naibu waziri wa maji Amos Makala kulia wakati akitoa maelekezo ya kurejea kazini baada ya kampuni hiyo kudaiwa kufanya mgomo wa kukataa kuendelea na kazi.PICHA/MTANDA BLOG
Mhandisi wa maji wilaya ya Mvomero Gabriel Ngongi kulia akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu waziri wa maji Amos Makala.
Wananchi wa kijiji cha KWADOLI.
Mwenyekiti wa kijiji cha KWADOLI, Yusuph Hamis akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa maji Amos Makala wakati waziri huo alipofanya ziara ya kukagua sekta ya miradi ya maji wilaya ya Mvomero.
Makala baada ya kuangalia mipira ya bomba kwa ajili ya kutandika chini ili kusambaza maji katika mradi wa maji kijiji cha KWADOLI.
Akizungumza jambo katika mkutano na wanakijiji wa Magadu ukumbi wa soko kuu la kijiji hicho
Mwandishi wa kituo cha Abood Media, Emmanuel Victor Mdoe akichukua habari katika ziara hiyo ukumbi wa soko kuu la Magadu.
Akizungumza jambo katika mkutano katika kijiji cha Magadu ukumbi wa soka.
Mkazi wa Magadu wilaya ya Mvomero, Said Hamad akizungumza jambo kwa naibu waziri wa maji katika mkutano uliofanyika ukumbi wa soko la kijiji hicho mara baada ya waziri huo kutembelea sehemu mbalimbali za miundombinu ya ujenzi wa visima vya maji.
Wananchi wakiagana na Naibu waziri wa maji mara baada ya kuongea nao katika ukumbi wa soko la Magadu.
Naibu waziri wa maji Amos Makala akimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Masalu Mayaya muda mfupi kabla ya kutembelea katika tanki la maji Kilosa.
Mhandisi wa maji wilaya ya Kilosa, Mathias Mwenda (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu waziri huku Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Masalu Mayaya.
Naibu waziri Makala akimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo.
Sehemu ya wanahabari katika ziara hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Gairo Hajat, Hanifa Karamagi akifafanua jambo ofisini kwake kwa Naibu waziri wa Maji Amos Makala mara baada ya kuwasiri wilaya ya Gairi.
Mbunge wa jimbo la Gairo Ahmed Shabiby akifafanua jambo mbele ya naibu waziri Amos Makala (hayupo pichani) muda mfupi kabla ya kutembelea vyanzo vya maji katika wilaya ya Gairo.
Makala akitembea kwa tahadhali wakati akielekea kutembelea chanzo cha maji cha Magongoko wilaya ya Gairo na maafisa mbalimbali wa serikali ya wilaya hiyo, kulia ni Meneja wa kampuni ya Serengeti Ltd, Askar Rahmani.
Naibu waziri wa maji Amos Makala kushoto akielekezwa jambo na Mbunge wa jimbo la Gairo Ahmed Shabiby kwa kumwonyesha chanzo cha maji kilichopo mlim Masenge ambacho kinaweza kutengwa mji ya mtiririko wakati wa ziara ya naibu waziri eneo la Ng'olongo kukagua miradi ya maji na kupokea taarifa ya upatikanaji wa huduma ya maji wilaya ya Gairi mkoani Morogoro. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Gairo Hanifa Karamagi.
Naibu waziri wa maji Amos Makala kushoto akielezwa jambo na Mhandisi mkazi Daktari, Josephat Singano katika eneo linapojengwa tanki la kusambaza maji la Magoeko katika mji wa Gairo .kutoka kushoto ni mbunge wa jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby na kulia ni Meneja wa kampuni ya Serengeti Ltd, Askar Rahmani.
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment