IRINGA.
NAIBU Katibu Mkuu wa (CCM)-Bara, Mwigulu Nchemba amewatakla wananchi wa jimbo hilo kumchagua Mgombea wa Chama hicho, Godfrey Mgimwa ili awaletea maendeleo yanayotokana na utekelezaji wa ilani ya chama hicho tawala.
NAIBU Katibu Mkuu wa (CCM)-Bara, Mwigulu Nchemba amewatakla wananchi wa jimbo hilo kumchagua Mgombea wa Chama hicho, Godfrey Mgimwa ili awaletea maendeleo yanayotokana na utekelezaji wa ilani ya chama hicho tawala.
Wakati CCM ikisema hayo, Mwenyekiti wa Baraza la
Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) John Heche
amesema, chama hicho kitasimamia maoni ya wananchi yaliyomo katika
Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza jana kwenye kampeni za uchaguzi katika
Kijiji cha Magubike na Nzihi Kata ya Nzihi, Nchemba ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Fedha alisema, anayeweza kusimamia utekelezaji wa ilani hiyo
ni Godfrey Mgimwa kutoka CCM.
Aliwataka Wanakalenga kuchagua mbunge anayetokana
na CCM ili kuendeleza na kukamilisha miradi ya umeme na maji ambayo
imeanza kutekelezwa tangu 2010.
Alisema Wanakalenga wakimchagua mbunge kutoka chama cha upinzani, wataendelea kupata shida zikiwamo za kukosa maji na umeme.
Naye Godfrey Mgimwa aliwaomba Wanakalenga kumpa
kura za ndiyo ili aweze kuungana na wabunge wengine katika kupeleka
maendeleo katika jimbo hilo lenye changamoto nyingi za elimu, afya na
mawasiliano.
Alisema yeye siyo mzungumzaji, bali ni mtendaji na
kuwa atafanya mambo mengi ikiwamo kutekeleza ahadi ambazo baba yake
alikuwa bado hajazitekeleza za madawati na uchangiaji wa ujenzi wa
zahanati na shule katika Kata za Kalenga.
Katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Ipamba,
Heche alisema, wameanza mchakato wa katiba kwa gharama kubwa, huku
akishangazwa na hatua ya CCM kuandaa waraka unaobadili mambo yote muhimu
yaliyoandikwa katika Rasimu hiyo na Tume ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa
Jaji Joseph Warioba.
Alitaja moja ya sababu ya chama hicho kuwataka
wamchague mgombea ubunge kupitia Chadema kuwa, CCM imeshindwa kuwaletea
maendeleo kwa zaidi ya miaka 50 tangu uhuru.
“Kila wakati wa uchaguzi, CCM huja na kutoa ahadi
lukuki kuwa tutawaletea maji, barabara, huduma za afya...leo viko wapi?
Tunaomba mumchague Grace, mjaribuni ili awaletee maendeleo,” alisema
Heche.
0 comments:
Post a Comment