Barca na Atletico Madrid watakutana kesho jumamosi kwenye uwanja wa Nou Camp

Wanaume wa kazi kesho wanavaana na Barcelona
KAMA Barcelona watashinda kesho dhidi ya Atletico Madrid na kutwaa taji la La Liga, siku inayofuata hawatakuwa na sherehe ya kushangilia ubingwa ndani ya basi lao la wazi na kupita mitaa ya Barcelona.
Hii inatokana na kushindwa kuonesha makali msimu huu, hivyo wanaona hakuna haja ya kufurahia mafanikio kiduchu namna hiyo.
Wachezaji, makocha, wakurugenzi na mashabiki wa Barca walishakata tamaa ya kutwaa ubingwa siku nyingi, kwahiyo kama watashinda kesho na kutwaa ubingwa wataondoka uwanjani ndani ya muda mfupi.
Wachezaji wa klabu hiyo wataondoka siku ya kesho yake na kwenda kujiunga na timu zao za taifa kujiwinda na michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

Anaondoka:
Carles Puyol aliitisha mkutano wa mwisho na waandishia wa habari alhamisi ya wiki hii na kutangaza kuondoka Barcelona

0 comments:
Post a Comment