BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA RAIS KIKWETE KUJENGA NYUMBA ZA MABALOZI KATIKA NCHI ZA ETHIOPIA, INDIA NA MISRI.

http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/06/Adam-Malima.jpgNaibu Waziri wa Fedha, Adam Malima.

SERIKALI inakusudia kujenga nyumba katika balozi zake nje ya nchi ili kupunguza gharama ya pango katika nchi wanazowakilisha.


Kauli hiyo ilitolewa bungeni mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima.

Alisema Serikali imefanya uamuzi wa makusudi kujenga nyumba hizo kutokana na kuwapo kwa viwanja vingi katika nchi hizo.

Alisema viwanja hivyo vilivyopo katika nchi za India, Ethiopia, Misri na kwingine vitasaidia kupunguza matumizi katika majengo ya ubalozi nje ya nchi kwa kuwa ina viwanja sehemu nyingi badala ya kila mwaka kukodisha.

“Tuna viwanja nchi nyingi badala ya kila mwaka kutumia shilingi milioni 14 hadi 15 katika pango ni afadhali tuanze kujenga huko, balozi anapopanga nje huwezi kuacha kumtumia fedha,” alisema Malima.

Alisema Serikali itatengeneza mfumo kudhibiti nidhamu katika matumizi ya fedha za umma.

Alisema vitu kama mbegu na mbolea katika sekta ya kilimo ni muhimu kwa sababu asilimia 70 ya Watanzania uhai wao unatokana na kilimo, hivyo Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko katika sekta hiyo.

“Tuna taasisi tatu za udhibiti wa mbolea, udhibiti wa dawa lazima tuhakikishe taasisi hizo zinapewa fedha za kutosha ili watu wasijitengenezee utajiri.

“Kuhusu uwekezaji wa miradi mikubwa, tumezungumzia miundombinu, reli, barabara na mawasiliano lakini kubwa zaidi ni kuhusu sekta ya umeme.

“Kwamba kwa mwaka huu, Serikali ipunguze matumizi yake katika nishati ya umeme na tuweze kuangalia utaratibu wa kukaribisha sekta binafsi kwa sababu tunatumia mabilioni ya fedha katika umeme sasa pale sekta binafsi itakapoingia ndiyo utaratibu wa nchi nyingine,” alisema Malima.

Kuhusu nafasi ya taasisi za fedha katika maendeleo ya nchi, alisema Serikali imekubaliana kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kufanya tathimini ya kiasi gani taasisi za fedha zinaweza kuchangia fedha nchini.MTANZANIA
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: