Na Mtanda Blog, Morogoro.
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi ameleza kuwa Tanzania inaweza kutwaa ubingwa wa bara la Afrika 2019 endapo tu mipango ya shirikisho hilo la kuendesha programu zake za usimamizi mzuri katika soka la vijana kuanzia miaka 13 hadi 17.
Akizungumza wakati akifunga mashindano ya Moro Youth-Kifimbo Cup 2014 katika uwanja wa jamhuri Malinzi alisema kuwa halitakuwa jambo la ajabu kwa Tanzania kutwaa ubingwa wa afrika 2014 kama kila idara ikifanya kazi kikamilifu katika mpango wa programu za kuendeleza mashindano ya vijana kuanzia 13 hadi 17.
Malinzi alisema kuwa Tanzania inakwama na kushindwa kufanya vizuri katika soka la kimataifa kwa sababu hakuna utamaduni wa kuwekeza katika soka la vijana hasa kuanzia umri mdogo.
“TFF kuanzia mwaka 2015 tutaanzisha mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 13, hadi 17 na lengo ni kutengeneza vijana wataokua na mfumo mmoja utaowezesha hata wachezaji wataochaguliwa timu ya taifa wasiwe na mashaka na mfumo wetu wa soka.”alisema Malinzi.
Aliongeza kuwa watafundishwa soka la mfumo mmoja utaoende sambamba na ule wa timu ya taifa na endapo progemu hiyo itaenda sawa ana matumaini mpaka mwaka 2019 Tanzania itakuwa timu ya kuotea mbali.
Malinzi alisema kuwa kazi iliyopo mbele yao kwa shirikisho hilo ni kuhakiki academ zinazoelewa watoto weenie vipaji na kuwaendeleza ili iwe kazi rahisi ya kuanzisha kwa mashindano hayo.
Aliendelea kueleza kuwa jukumu lingine ni lazima katika academ hizo kuwe na walimu wa soka wenye ujuzi wa kutosha ili mpango huo uende sawia na mpango wa TFF.alisema Malinzi.
0 comments:
Post a Comment