Mbeya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi, amewataka wanafunzi nchini kuwa makini na ulaji wa mikate na pipi au vinywaji mbalimbali kwani upo uwezekano wa kuwekewa dawa za kulevya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi, amewataka wanafunzi nchini kuwa makini na ulaji wa mikate na pipi au vinywaji mbalimbali kwani upo uwezekano wa kuwekewa dawa za kulevya.
Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani,
Iringa, alitoa rai hiyo juzi wakati akizungumza machache wakati wa
kumkaribisha Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal kwenye maadhimisho
ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya duniani ambayo
kitaifa yalifanyikia mkoani Mbeya.
Alisema wapo watu wenye nia mbaya kwa wanafunzi na
wanabuni mbinu ya kuwawekea kidogo kidogo dawa za kulevya kwenye mikate
na pipi, vitumbua, maandazi na kwenye vinywaji kama vile juisi kwa
lengo la kuwazoesha na matumizi ya dawa hizo.
“Kuweni waangalifu na mikate na pipi, soda na
juisi mnazoletewa shuleni kwenu, kwani kuna watu wenye lengo la
kuwazoesha kutumia dawa za kulevya kwa kuwawekea kidogokidogo,” alisema
Lukuvi .
Lukuvi pia alisema wako vijana 403 wanaoshikiliwa
nje ya nchi kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya na kwamba hakuna
uwezekano kwao kurejea nchini kwani watahukumiwa kwa mujibu wa sheria za
nchi hizo.
‘’Hawa vijana watahukumiwa kufungwa maisha na
wengine watahukumiwa kunyongwa tu hawatarudi, hivyo ni lazima vijana
mkaacha kutumika na vigogo na katika biashara hii’’,alisema.
Awali, Makamu wa Rais akihutubia alisema Serikali
imewavalia njuga watu wanaojihusisha na usambazaji wa dawa za kulevya na
kwamba inachohitaji ni wananchi kutoa taarifa.
Dk Bilal alisema tangu 2009 hadi sasa watu 13,846
wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya na kwamba tani
212 za bangi nazo zilikamatwa, huku kilo 969 za heroini zilikamatwa na
cocaine kilo 363.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment