HII NI MOJA YA SIFA YA POMBE ISIYOFAA NDANI YA JAMII.
Ulevi umetajwa kuwa moja ya chanzo cha ubakaji na unyanyasaji wanawake na watoto kingono, unaofanywa katika jamii nyingi nchini.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa), wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, matumizi ya pombe miongoni mwa wanaume yamesababisha ubakaji na unyanyasaji wa wanawake na watoto majumbani na mitaani.
Ili kupambana na tatizo hilo Tamwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inatekeleza mradi wa miaka mitatu wa kuwahamasisha watu kuachana na ulevi na matumizi ya pombe kwa kuwa imeonekana kuwa ni njia mojawapo inayochangia unyanyasaji wa kijinsia hasa wa ngono.
Lengo la mradi huo ni kupunguza unywaji pombe, ukatili dhidi ya wanawake na watoto na hatimaye kutungwa kwa sheria ndogo ndogo kupunguza na kutokomeza ulevi katika jamii.
Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa Valerie Msoka, alisema mradi huo utaanzia katika wilaya ya Kinondoni ambayo imekuwa na matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yanayotokana na unywaji wa pombe na baadaye utaelekezwa katika wilaya zingine.
Pamoja na changamoto hiyo alisema ubakaji unasababisha kupata mimba sizizotarajiwa ambao unachangia utoaji wa mimba hizo ama kuwatelekeza watoto wanaozaliwa na kuishia kuishi mitaani.
Licha ya licha ya watoto hao kuishi katika mazingira magumu hasa mitaani wengi wakikosa huduma muhimu na kuongeza idadi ya maskini. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
0 comments:
Post a Comment