Mario Götze anaipatia Ujerumani bao la ushindi.
Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia.
Ijapokuwa alishindwa kutwaa ubingwa wa dunia Lionel messi alitawazwa kuwa Mshindi wa tuzo la ''Golden Ball''.
Makala yajayo ya kombe la dunia yataandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.
Putin alipewa ithibati rasmi ya kuwa mwenyeji wa makala yajayo ya kombe la dunia la mwaka wa 2018.
00:25 Mario Gotze anaiweka Ujerumani mbele
00:24 GOOOOOOOOAL
00:08 Palacio anapoteza nafasi nyengine huku Messi akionekana kulemewa na walinzi wa Ujerumani.
Argentina 0-0 Ujerumani 90''.
Sasa ni Muda wa Ziada (Extra Time)
00:90 Argentina 0-0 Ujerumani 90''.
00:90Muda wa kawaida umekamilika katika fainali hii .
00:86 Joachim loew anajibu kwa kumuingiza Gotze
00:85 Argentina inajiandaa kufanya mabadilikokatika safu ya kati Gago anaingia
00:80 Krooooooooos anapoteza nafasi nyengine
00:70 Ujerumani inakosa tena Schurrle
00:60 Argentina 0-0 Ujerumani 60''.
00:58 Argentina 0-0 Ujerumani
00:48 Goalkick kuelekea upande wa Argentina
00:46 Messi anapoteza nafasi nyengine
22:45 Sergio Aguero anaingia badala yake Ezequiel
22:45 Ujerumani 0-0 Argentina
22:45Kipindi cha pili kinaanza huko Maracana
22:45 Ujerumani wanapoteza nafasi nzuri.
mkwaju wa kichwa unapogonga mwamba na msaidizi wa refarii anasema ni Offside kwa Thomas Muller
22:39 Lionel Messi ananyimwa fursa ya kufanya mashambulizi
22:37 Ujerumani wanafanya shambulizi lingine .
22:35 Higuan anafunga lakini refarii anakataa anasema aliotea .
22:20 Gonzalo Higuan apoteza nafasi ya wazi akiwa amesalia pekee yake na na kipa Nuer
22:18 Ujerumani 0- 0 Argentina 20''
22:14 Kona kuelekea upande wa Argentina.
22:13Freekick kuelekea lango la Argentina lakini wapi unagongwa nje na unakuwa wa kurushwa kuelekea Argentina.
22:10 Kona ya kwanza katika mechi hii kuelekea upande wa Ujerumani
22:09 Messi anaongoza shambulizi hadi ndani ya eneo la lango lakini mjerumani hapishi.
22:03 Argentina wanashambulia lango la Ujerumani lakini wapi .
22:01 Freekick kuelekea lango la Argentina .
22:00 Mpira umeanza .
Timu zimeingia uwanjani tayari kwa fainali hii.
Wimbo wa taifa wa Ujerumani unapigwa kisha ule wa Argentina .
Vijana wa Joachim Loew wanamtarajia mfungaji wao nyota Miroslav Klose akisaidiana na Thomas Muller kuwapa mabao na hatimaye ushindi dhidi ya Argentina.
Kwa Upande wao Ujerumani imesifiwa kwa kuwa na uwezo wa kipekee wa kucheza kama kikosi wala sio kumtegemea nyota mmoja kwa ufungaji mabao.
Argentina nayo inakumbuka vyema matukio ya miaka 28 iliyopita ilipoilaza Ujerumani Magharibi wakati huo na kutwaa kombe lao la mwisho la dunia
Ujerumani ilishinda mara moja nayo Argentina ikaibuka mshindi mara moja kwa hivyo hii leo itakuwa mechi ya kukata na shoka.
Wajerumani wakiandikisha rekodi kwa kuinyeshea wenyeji Brazil jumla ya mabao 7-1 katika nusu fainali huku Argentina nayo ikihitaji muda wa ziada na hata mikwaju ya penalti kuibandua Uholanzi na kufuzu.
Timu hizi zimechuana mara 2 katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 1986 na 1990.
Hayo yote ni kenda timu hizo zote zilikuwa zikiwania kuandikisha majina yao kwenye tuzo la kipekee la dhahabu yaani kombe la dunia.
Mechi hiyo ndiyo itakayokuwa kilele cha majuma manne ya kipute hicho kilichojumisha timu 32 kutoka mabara yote 5 zikichuana miongoni mwao katika miji 12 ya Brazil kuanzia juni tarehe 12 .
Macho yote duniani yanaelekea katika uwanja wa Maracana ulioko Rio Brazil ambapo mechi ya fainali ya kombe la dunia itachezwa muda mchache ujao.
Jumapili ya tarehe 13 Julai mwaka wa 2014 hatimaye imewadia.
0 comments:
Post a Comment