Tarime. Mkaguzi Mkuu wa Shule za Msingi wilayani Tarime Josephu Mowinga ameifungia Shule ya msingi Kegonga iliyopo kata ya Kegonga baada ya kubainika haina choo kwa muda mrefu.
Mkaguzi huyo Mkuu wa wa Shule za Msingi wilayani Tarime Joseph Mowinga alisema kuwa chanzo cha kufungiwa kwa shule hiyo ni kutokana na wananchi kutochangia shughuli za shule na kusababisha wanafunzi kukosa vyoo.
Aliitaka Jamii wilayani Tarime mkoani Mara kuwa na mwamko na kushirikiana na Serikali kuboresha shule ili watoto wasisome kwenye mazingira hatarishi na kwamba kutochangia maendeleo ya shule kunashusha taalauma kwa wanafunzi.
Mowinga alisema kuwa shule hiyo inawanafunzi 512 wavulana 267 na wasichana 245 ambapo majengo hayo yanatumiwa pia na wanafunzi wa shule ya Nyandage yenye jumla ya wanafunzi 684 wavulana 316 na wasichana 368, hivyo jambo la kukosa vyoo ni hatari kwa afya zao.
“Tumeifungia shule kwa kukosa choo, kwani vyoo vilivyokuwepo vilikuwa vibovu vilijengwa kwa kulaza miti na kukandikwa kwa udongo na kubomoka Halmshauri ilitoa Sh5.8 milioni, lakini yamechimbwa matundu 12 fedha hazikutosha kukamilisha ujenzi na hakuna nguvu yoyote ya wananchi iliyotumika kwenye ujenzi kwahiyo tumeifungia ili wananchi wakamilishe ujenzi”alisema Mowinga.
Diwani wa Kata ya Nyanungu Ryoba Mangeng’i (Chadema) alisema kuwa baaa ya kufungiwa kwa shule hiyo wananchi wamejitokeza kuchangia fedha ili kukamilisha vyoo nakwamba ujenzi unaendelea na ndani ya siku 14 vyoo vitakuwa vimekamilika.
Mlezi wa shule ya Msingi Nyanungu ambaye pia ni Ofisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Selvanus Gwiboha alisema kuwa hadi sasa wananchi wamechangia milioni moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment