KAMPUNI YA APPLE YAINGIZA BIDHAA MPYA SOKONI, NI SAA INAYOTUMIA PROGRAMU.
Wataalamu wanasema kuwa Apple husukuma teknolojia katika anga za juu na kuibuka na vitu vya aina yake.
Kampuni ya Apple imezindua saa mpya aina ya smartwatch ijulikanayo kama 'The Apple Watch'.
Huu ni uzinduzi wake wa kwanza wa bidhaa nyinginezo nzuri tangu kufariki kwa mwanzilishi wa kampuni hiyo Steve Jobs.
Saa hiyo inatumia programu na pia ni kama kifaa cha kumsaidia mtu kujiweka katika hali nzuri ya kimwili kwa kuangalia mazoezi anayofanya na hata kumshauri mtumiaji, kwa kuwasiliana na simu yake ya iPhone.
Wakati simu nyingine kama hizo tayari zikiwa sokoni, wataalamu wanasema kuwa kampuni ya Apple ina historia ya kuingia katika sekta mbali mbali kwa kuchelewa lakini kikubwa ni kuwa huwa inabadilisha teknlojia na kuja na vitu vipya.
Apple pia ilizindua simu zake mbili mpya ambazo ni kubwa ikilinganishwa na simu zake za awali.
Skirini ya iPhone 6 ina upana wa nchi 4.7 huku iPhone 6 Plus ikiwa na skrini yenye nchi 5.5.
Haya ni mabadiliko ambayo wadadisi wanasema inawazuia wateja wa Apple kuhamia kwenye simu zenye mfumo wa Android.
Kampuni hiyo pia ilitangaza, huduma mpya ijulikanayo kama Apple Pay, ambayo mkurugenzi wake anasema wanatumai itakuwa kama mfuko wa mtu kubeba pesa.
Saa ya Apple ina sura 11 na huruhusu mtumiaji kubadili mikanda yake.
0 comments:
Post a Comment